Header Ads Widget

JOPO LA WANASAYANSI LAADHIMIA KUENDELEA KUFANYA UTAFITI WA MAHUSIANO YA PANYA NA VIUMBE WENGINE

 



Teddy Kilanga_ARUSHA



Jopo la wanasayansi kutoka nchi 50 Duniani wameadhimia kuendelea kufanya utafiti wa mahusiano ya  mnyama panya  pamoja na viumbe vingine vilivyopo katika mazingira yake kutokana na umuhimu wake.



Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo Mwenyekiti wa mkutano huo, ambaye ni Mtaalamu wa Utafiti wa Ikolojia ya Panya kutoka Kituo cha Umahiri cha Utafiti wa Panya cha chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Prof. Rhodes Makundi alisema inaelekea panya kuwa na umuhimu katika magonjwa na kilimo.



"Panya anaelekea kuwa muhimu katika magonjwa na kilimo hivyo ni lazima tuendelee kufanya utafiti wa kina zaidi ikiwa sasa tumetambua utafiti wa kuzuia panya kuzaana kwani katika Afrika Tanzania ndio inayoongoza kwa utafiti huu,"alisema Profesa Makundi.



Aidha aliongeza kuwa katika mada walizojadili ni pamoja na kutumia njia za kuzuia uzazi wa panya hali itakayosaidia wakulima kuounguza idadi ya Panya mashambani kwao na hata majumbani.



Alisema njia hiyo wataitumia aina ya homoni itakayochanganywa kwenye chakula cha panya na kuweza kuzuia panya asipate mimba na panya dume asiweze kumpa panya jike mimba ikiwa njia hiyo itapinguza hasara kwa wakulima ambao mazao yao huliwa na mnyama huyo.




Profesa Makundi alisema eneo lingine lenye umuhimu katika utafiti ni matumizi ya panya kwa faida ya binadamu kwa utambuzi wa mabaomu na magonjwa kama kifua kikuu hivyo wanaendelea na utafiti.



Pia alisema  jopo la Wanasayansi hao limetambua mchango wa baadhi ya maprofesa  kwa kazi nzuri waliyoifanya kusaidia binadamu kuondoa matatizo ya Panya ambapo wamepewa tuzo mmoja wapo akiwa ni yeye Profesa Rhodes Makundi kwa kufanya kazi kwa takriban  miaka 40 pamoja na wengine wawili ambao wamefanya kazi kwa takriban miaka 30 ambapo mkutano huo umehudhiriwa na watu zaidi ya 100 huku zaidi ya 80 wakishiriki kwa njia ya mtandao.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI