Header Ads Widget

"JESHI LA POLISI LINATAMBUA MCHANGO WA KILIMO NCHINI"_ IGP SIRRO

 



Na junior Mwemezi TARI makao makuu


Kamanda wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro amesema   Jeshi la Polisi linatambua mchango wa kilimo nchini na umuhimu wa utafiti katika kuendeleza kilimo kupitia  Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) na wadau wengine katika mnyororo wa thamani .


Kamanda Sirro ameyasema hayo leo alipotembelea mabanda ya TARI ili kuona shughuli za utafiti na mchango wake katika kutekeleza Agenda 10/30  ya Kilimo ni Biashhara, ambapo kilimo kinatarajia kukua kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.



"Nafarijika na maelezo yaliyotokewa kuhusu umuhimu wa kufahamu afya ya udongo kabla ya kuanza kilimo cha zao lolote ili kusaidia maamuzi ya kiasi na aina ya mbolea kulingana na zao. Alisema, TARI iongeze nguvu katika kuwashauri wakulima ili kuongeza uelewa na kukifanya kilimo kuwa chenye tija" amesema kamanda Sirro .


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Dr Geoffrey Mkamilo ametoa hakikisho kuwa  TARI itaendelea kusambaza teknolojia za kilimo kwa wananchi na kuwasaidia kulima kilimo chenye tija.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI