.
Na MatukioDaimaAPP, Dar es Salaam
CHAMA cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala kimepata pigo kufuatia Diwani wake wa Kata ya Mahohe Mohamed Ngonde, kufariki leo alfajili
Akizungumza kwa njia ya simu Katibu wa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Busoro Pazi, alisema Marehemu Mohamed Ngonde alifariki akiwa
katika Ibada ya alfajiri Leo Julai 08/2022 akiwa msikitini.
Katibu wa Madiwani Busoro Pazi alisema taratibu za mazishi bado kila wakati atakuwa anatoa taarifa baada kukaa na familia ya marehemu.
"Kwa Sasa tunafanya taratibu za kwenda kuifadhi mwili wa marehemu katika hospitali ya Rufaa Mkoa Amana "amesema Busoro.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde alisema taarifa za Kifo cha MH, Diwani wake Mohamed Ngonde aliyefariki alfajili katika alizipata kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM kata Majohe ambapo alisema alimweleza kuwa Marehemu Mohamed Ngonde alifariki ghafla.
Mwenezi CCM Wilaya ya Ilala Alhaj Said Sidde amesema kila wakati atakuwa anatoa taarifa kamili kuhusiana na msiba huo mzito kwa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na wana CCM kwa ujumla.
Alhaj Said Sidde,pia ongeza kuwa amemwelezea Ngonde kuwa kada mahiri aliyekitumikia Chama Cha Mapinduzi kwa muda mrefu na kushikilia nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mwenyekiti serikali ya mtaa Kichangani ,Majohe
0 Comments