NA CHAUSIKU SAID , MATUKIODAIMAAPP MWANZA.
Zaidi ya vijana 50 Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza wamepata ajira kutoka katika kampuni ya uuzaji wa vifaa vya uchimbaji madini Rock Solution.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Rock Solution Zacharia Nzuki alipokuwa akizungumza na matukio daima na kueleza kuwa tangu mwaka 2015 kuanzishwa kwa kampuni hiyo wamekuwa wakiajili vijana wazawa wa wilayani hapo na kuweza kunufaika na ajira hiyo.
Nzuki amesema kuwa lengo la kuanzisha kampuni hiyo ni pamoja na kuongeza kipato kwa Taifa, ajira kwa wazawa wa wilaya hiyo ili waweze kujimudu kimaisha na kuachana na makundi yasiyo satahili katika jamii hali inayowafanya vijana wengi kujiingiza katika wizi na utumiaji wa madawa ya kulevya.
Amefafanua kuwa mbali na kuanzisha kampuni ya uuzaji wa vifaa vya uchimbaji madini pia wameanzisha ujenzi wa kiwanda kitakachozalisha vifaa vya utafiti kwenye migodi yote hapa nchini pia kuongeza ajira takribani 200 kwa vijana 200 ambao bado wako nyumbani.
"Sisi kama Rock Solution tuliona badala ya kuendelea kuchukua vifaa ulaya wakati sisi tunaweza tukawashawishi wawekezaji badala ya kwenda kununua kule waje wawekeze hapa nchini" Alisema Nzuki.
Nzuki amesema kuwa mbali na huduma hizo wanazozitoa wamekuwa wakihudumia wananchi kwa mahitaji mbalimbali ikiwemo ujimbaji wa kisima kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha mayolwa pamoja na ujenzi wa msikiti, kanisa, zahanati na shuleni kutoa misaada ya vitabu pamoja na kutoa misahada kwa watoto yatima na wanaoishi katikaazingira magumu.
Aidha amempongeza Rais Samia kwa kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wazawa wa makapuni hali ambayo hali ambayo itawafanya kufanya kazi zao kwa mazingira mazuri.
"Ukimwezesha mwekezaji mazawa utakuwa umewawezesha vijana wengi kupata ajira kirahisi" Alisema Nzuki.
Nae kwa upande wake meneja Mkuu wa Rock Solution Fabian Mayenga amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikitoa ajira kwa vijana wote bila kuwa na ubaguzi wa aina yeyote ile iwe wa rangi ama ulemavu wa viungo.
" hapa tunafanya kazi na watu wote hatuna tabia ya kubagua tunamchukua mtu wenye ujuzi na kazi yake hata kama akiwa mlemavu lakini anaujuzi na kazi hiyo sisi tunamuajili" Alisema Mayenga.
Mayenga amesema kuwa zaidi ya watoto wapatao 50 wanaoishi katika vituo vya kulelewa wamekatiwa bima ya afya na kampuni hiyo ambapo zitawasaidia katika swala zima la afya.
Hata hivyo ametoa wito kwa watu wenye makapuni binafsi na vikundi wawe na mazoea ya kujitoa katika kuwahudumia watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea pamoja na wanaoishi katika mazingira magumu ili na wao waweze kuwa na furaha kama watoto wengine.
" mimi niseme tu watu binafsi wenye uwezo na makapuni waone kuwahudumia watoto yatima na wasiojiweza ni moja ya sadaka, ukijiweka wewe mwenyewe kqa kuangalia leo mimi nipo je nikiwa sipo familia yangu itahudumiwa na nani" Alisema Mayenga.
0 Comments