Na Gabriel Kilamlya NJOMBE
Mkoa wa Njombe Wenye Vyanzo Vya Maji Vinavyopindukia 4436 Vimetakiwa Kuendelezwa kutunzwa Kwa Kupanda Miti rafiki na Maji Ili Kuendeleza Uhifadhi wa Mazingira na Kuboresha Upatikanaji Maji.
Hii Inatajwa Kwenda Kupunguza Changamoto Kubwa ya Uhaba wa Maji na Kutunza Mazingira ambayo yameonekana Kuharibiwa Pakubwa Kwa Kuendeleza Shughuli za Kilimo,Mifugo na Hata Kujenga Makazi Katika Maeneo Oevu.
Katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Yaliyofanyika Kimkoa Katika Eneo Oevu Lililopo Hagafilo Mjini Njombe Kwa Kupanda Miti Aina ya Mivengi Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa Kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa Waziri Waziri Kindamba Amepiga Marufuku Kuendeleza Shughuli zozote Katika Maeneo ya Vyanzo Vya Maji.
Awali Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Judica Omary Amesema Wanapanda Miti Hiyo Rafiki na Mazingira Ili Kuongeza Uimarishaji wa Uhifadhi wa Mazingira Katika Bonde la Nyikamtwe Huko Lunyanywi.
Diwani wa Kata ya Mjimwema Nestory Mahenge na Laurent Lupenza Mweyekiti wa Mtaa wa Lunyanywi Wanaahidi Kuitunza Miti Hiyo kwa Maslahi Mapana ya Vizazi Vijavyo.
Baadhi ya Wakazi wa Mtaa Huo Walioshiriki Zoezi la Upandaji Miti Hiyo Akiwemo Baraka Kunga na Conslatha Kitule Wanakiri Kuwa Eneo Hilo Lilianza Kuvamiwa na Baadhi ya Wakazi na Kwamba Hatua Iliyochukuliwa na Serikali ya Upandaji Miti Hiyo Itasaidia Sana Kuhifadhi Mazingira ya Bonde Hilo.
Kauli Mbiu ya Siku ya Mazingira Duniani Kwa Mwaka Huu Inasema''TANZANIA NI MOJA TU,TUNZA MAZINGIRA'' Ambapo Jumla ya Vyanzo 512 Mkoani Njombe vimehifadhiwa kwa njia Mbalimbali ikiwemo Kuzungushia Uzio.
0 Comments