Header Ads Widget

WAKULIMA WA KOROSHO WASISITIZWA KUFUATA KANUNI BORA ZA KILIMO

 




NA HADIJA OMARY MATUKIODAIMA APP _LINDI……..



TAASISI ya Utafiti wa mazao Tanzania (TARI Naliendele) iliyopo Mkoani Mtwara imewashauri wakulima wa zao la korosho kufuata kanuni nyingine za kilimo bora cha zao hilo , hususani matumizi ya mbegu bora, kupanda kwa nafasi, kuchanganya korosho na mazao ya msimu, palizi na upogoleaji zinazoshauriwa na wataalamu.


Ushauri huo umetolewa na ofisa uhaulishaji wa Teknolojia na mahusiaano kutoka Taasisi hiyo Emmanuel Mgimiloko wakati wa mafunzo ya matumizi sahihi na salama kwa maafisa ugani wa halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.


Mgimiloko alisema kuwa pamoja na Udhibiti wa visumbufu vya zao la korosho (wadudu waharibifu na magonjwa) kuwa ni miongoni mwa kanuni za kilimo bora cha zao hilo, ili kuweza kuongeza tija na uzalishaji nchini jambo hilo ni muhimu pia kuzingatiwa.

 

Alisema ili kuendelea kupambana na changamoto za magonjwa pamoja na wadudu waharibifu ni muhimu kwa wakulima wa zao Korosho kuzingatia kanuni bora za kilimo cha zao hilo kama inavyoshauriwa na wataalamu hao.


Aliongeza kuwa kwa kutumia kanuni tofauti tofauti za kilimo zinazoshauriwa na wataalamu wakulima hao wanaweza kumaliza changamoto za zao hilo kwa rahisi na haraka Zaidi.


Hata hivyo Mgimiloko alisema kuwa ushiriki kikamilifu wa viongozi na wasimamizi wa tasnia ya korosho nchini katika kuhamasisha uwajibikaji, kutaongeza tija kubwa katika uzalishaji wa zao la korosho nchini.


Kwa upande wake ofisa kilimo na umwagiliaji wilaya ya Ruangwa Nolasco kidumile aliishukuru Taasisi hiyo ya TARI Naliendele kwa jitihada wanazozifanya katika kuwakumbusha maofisa ugani juu ya maswala mbali mbali yanayohusu zao hilo la korosho .


“katika zao la korosho kwa TARI sisi wilaya ya Ruangwa tunatambua sana mchango wao Mfano katika msimu uliopita  wilaya yetu ilifanikiwa kuongeza uzalishaji kutoka tani 10,700 hadi kufikia 13,188 kwa msimu wa mwaka 2021/2022”.


Hata hivyo Kidumile aliongeza kuwa  kwa Wilaya ya Ruangwa mafunzo hayo ya matumizi sahihi ya viuwatilifu kwa maofisa ugani yamefika wakati muafakwa kwa kuwa sasa ndio halmashauri hiyo ipo katika zoezi la ugawaji wa pembejeo za zao hilo

 

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI