Header Ads Widget

VIONGOZI WA DINI NA TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI ZATAKIWA KUWAHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI.

 


Na Chausiku Said, Mwanza


Viongozi wa dini Mkoani Mwanza kwa kushirikiana na Taasisi za umma na binafsi zilizopo mkoani hapa zimetakiwa kuunga mkono serikali kwa kuweka mabango yenye jumbe za kuhamasisha wananchi Kushiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi inayotarajia kufanyika Agosti 23 mwaka huu.


Rai hiyo imetolewa na katibu tawala Mkoa wa Mwanza Ngussa Samike wakati akizungumz na viongozi wa kamati ya Amani kutoka madhehebu ya kiislam na kikristo katika ukumbi wa Mwanza hoteli na kusema Taasisi hizo na viongozi wa dini kuweka jumbe za matangazo kwenye nyumba za ibada kwa kuwapa elimu waumini juu ya sensa na kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa kwa kushirikiana na makarani wa sensa.



Samike amesema lengo la sensa ya watu na makazi ni kupata taarifa sahihi za kidemografia,kijamii,kiuchumi na hali ya mazingira kwa lengo la kupata takwimu zitakazowezesha Serikali na wadau wengine kupanga maendeleo ya watu katika sekta muhimu za afya,Elimu,Nishati na Madini,Miundo mbinu na maji Safi.


"Sensa ya watu na makazi ni moja ya zoezi muhimu linalokusanya taarifa za Kila mtu aliyelala ndani ya mipaka ya nchi taarifa hizi zitahusu Kidemografia, taarifa za Kilimo Mifugo Uvuvi na Misitu,taarifa za Uzazi,Ulemavu, Elimu, taarifa za Kiuchumi,huduma za kijamii pamoja na anwani za makazi"amesema Samike.



Ameongeza kuwa umuhimu wa sensa hauishii serikalini unaenda mpaka kwenye ngazi ya chini ya jamii ambayo viongozi wa dini wanaziongoza.


"Nawapongeza Sana kwa jitihada ambazo mmefanya, sisi tunapopoke Wito wowote kutoka kwa viongozi wa dini tuko tayari katika ngazi ya Mkoa nawapongeza kwa ushirikiano ambao mkonao kuanzia katika ngazi ya uongozi wenu mpaka katika ngazi za chini huu ushirikiano mlionao  na serikali tunashukuru Sana"amesema Samike.


Kwa upande wake Askofu Charles Sekerwa amesema sensa itasaidia kujua idadi ya watu,maendeleo,mikakati na ubora wa uongozi.



"Sisi Kama viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali ya kikristo na kiislam tupo bega kwa bega na Raisi wetu tunaahidi tutakuwa mabarozi wazuri kwa kuwahimiza waumini wetu Kushiriki vyema katika zoezi Zima la sensa ya watu na makazi" amesema Askofu Sekerwa.


Nae Sheikhe Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke amesema tumeshaanza kuelimisha waumini wa dini zote juu ya sensa ya watu na makazi tumetembea wilaya zote za mkoa wa Mwanza kuelimisha waumini katika zoezi Zima la sensa.



"Tulishaanza kuelimisha Jambo hili lakini tukaona bado sisi ni namba mbili maana wewe ulituelimisha sisi na sisi tunawaelimisha wenzetu tukaona ni vizuri kamati ya amani kutafuta uwezekano wowote ili tuje kuwaita viongozi wetu na wewe uje uzungumze nao"amesema Sheikhe Kabeke.


Kwa upande wake mratibu wa sensa wilaya ya Nyamagana  Ruhinda Costantine amesema kuwa sensa ya watu na makazi itasaidia serikali kufahamu matatizo yaliyopoya na namna ya kuweza kuzitatua.



Ameongeza kuwa  sensa hiyo itahusisha makarani wa sensa ambao watatembea kaya zote nchini na kufanya mahojiano na Mkuu wa kaya ambao watawasaidia kupata takwimu sahihi ili kukamlisha zoezi hilo.


Sanjari na hayo amesema sensa ya watu na makazi itasaidia kupata taarifa ya kujua idadi ya wanaume na idadi ya wanawake, umri, hali ya ndoa (kidemografia), kujua taarifa za kijamii, uchumi, na hali ya mazingira kwa lengo la kupata takwimu sahihi ambazo zitawezesha Serikali Kupata taarifa za maendeleo,kisiasa, hali ya  kibiashara pamoja na kuandaa bajeti na kuleta mahitaji kwa wananchi.


Baadhi ya viongozi wa dini Sheikhe  Abdulwarith Juma Abdallah na Mchungaji Ester Raymond wamesema mafunzo hayo yamewasaidia kwenda kuwaelimisha waumini umuhimu wa sensa.


"Tumepata Elimu viongozi wa dini tuwafikishie jamii wajue umuhimu wa sensa wale watu tulionao tuwafundishe na bila sensa huwezi kujua yatima,wajane,watu kwenye nyanja na Idara mbalimbali bila sensa,wafanyakazi, wafanyabiashara,wakulima,wavuvi bila sensa.


Hata hivyo wamewomba watanzania kujitokeza katika kushiriki kikamilifu katika sensa ya watu na makazi kwa ajili ya kuliletea taifa maendeleo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI