Header Ads Widget

UWT KILIMANJARO WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUPATA TUZO YA BABACARNDIAYE.



NA WILLIUM PAUL, MOSHI.


UMOJA wa Wanawake wa chama cha Mapinduzi (UWT) mkoa wa Kilimanjaro umesema kubwa tuzo ya Babacarndiaye aliyoipata Rais Samia Suluhu Hasani nchini Accra Ghana amestahili kwani amefanya mambo makubwa katika kipindi chake cha mwaka mmoja cha Urais wa Tanzania.


Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Kilimanjaro, Zuhura Chikira wakati akitoa tamko la Wanawake wa mkoa wa Kilimanjaro kumpongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu Hasani.



Chikira alisema kuwa, katika uongozi wa awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hasani yapo mambo makubwa ambayo ameyafanya lengo likiwa ni kuhakikisha anawaletea wananchi maendeleo.


"Ni mwaka mmoja sasa tangu Samia Suluhu Hasani awe Rais lakini ameweza kuifungua nchi yetu kimataifa na kuifanya ijulikane ulimwengu mzima hivyo tuzo aliyoipata imemstahili kwa jinsi anavoongoza" alisema Zuhura.


Alisema kuwa, kwa sasa Dunia imetambua kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia hata kupelekea kumpa tuzo ya Babacarndiaye ambapo ni heshima kubwa kwa Taifa la Tanzania.



Mwenyekiti huyo alidai kuwa, wakinamama wa mkoa wa Kilimanjaro wataendelea kumuunga mkono katika juhudi zake za mapambano ya kuleta maendeleo.


Aidha Mwenyekiti huyo alitumia pia nafasi hiyo kuwaasa wakinamama wa mkoa wa Kilimanjaro kushiriki kikamilifu katika sensa ya watu na makazi kwa kutoa takwimu sahihi lengo ni ili Serikali iweze kupata takwimu sahihi za wananchi wake iweze kuwahudumia.


Kwa upande wake, Katibu wa UWT mkoa wa Kilimanjaro, Irimina Mushongi aliwataka wananchi kuhakikisha wanaitunza na kuilinda miradi na miundombinu inayojenga na Serikali ili iweze kudumu muda mrefu.



Irimina alisema kuwa, kwa upande wa sekta ya Afya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hasani imefanya mambo makubwa ikiwamo ujenzi wa hospitali, vituo vy afya pamoja na zahanati lengo likiwa ni kuwasogezea wananchi huduma karibu.


Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI