Na John Mapepele
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameipongeza
timu ya Yanga kwa kutwaa kombe la katika ligi Kuu ya NBC katika msimu
huu.
Mhe. Mchengerwa
ameipongeza Klabu ya Yanga kwa kuchukua Ubingwa huo huku akipongeza
mshikamano na furaha za mashabiki, ambazo wamezionyesha wakati wa
kukabidhiwa kombe hilo na mapokezi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
"
Kwa aina ya shangwe za ubingwa zilizofanyika jana na leo ni sawa na
zile za mataifa yaliyoendelea ya Ulaya. Hakika mpira wa miguu ni mchezo
mkubwa na pendwa duniani ambao huwaunganisha watu pamoja na kuleta
amani, mshikamano, furaha na umoja baina ya wananchi"
Ameongeza
kuwa watanzania zaidi ya 90% ni wapenzi wa mchezo wa soka na
amesisitiza kuwa serikali itaendelea kufanya kila linalowezekana
kuhakikisha inaboresha miundombinu ya michezo na kuleta usawa katika
michezo hasa mpira wa miguu ili kila mtanzania aweze kupata furaha.
"Serikali
ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan,
itafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa watanzania wanaendelea
kupata furaha na faraja katika michezo" amesisitiza Mhe . Mchengerwa
0 Comments