Header Ads Widget

TANTRADE NA DART KURAHISISHA USAFIRI MAONESHO YA SABASABA


**************************

Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) imesema kuwa maonesho ya mwaka huu wamejipanga kuondoa adha ya usafiri ambapo wananchi wataweza kutumia mabasi yaendayo haraka (DART) kutoka Gerezani hadi Sabasaba.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Latifa Khamis wakati wakitiliana saini ya makubaliano na Wakala wa mabasi yaendayo haraka DART ambapo amesema tiketi za kuingia katika maonesho hayo zitakua zinapatikana katika vituo vya Dart lengo ni kurahisisha usafiri na kuondoa msongomano.

Amesema kuwa, makubaliano hayo yamekuja kutokana na shida ya usafiri inayokuepo kipindi chote cha maonesho, hivyo wananchi wamerahisishiwa huduma ya usafiri.

Aidha, amesema wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha wanaleta kitu kipya kila mwaka wa Maonesho ya Sabasaba hivyo kwa mwaka huu wameamua kuleta suala la urahisishaji wa usafiri kwa washiriki wa Maonesho hayo.

"Washiriki wa Maonesho wataweza kuchukuliwa kutoka kituo cha Gerezani moja kwa moja na kuletwa hapa katika Maonesho ya Sabasaba, tunataka wananchi watambue kuna urahisi wa kufika na kuondoka hapa kupitia mabasi ya DART"amesema Latifa.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo kwa haraka (DART), Dkt.Edwin Muhede amesema kutakuwa na maegesho ya magari katika maeneo maalumu waliyoyaandaa ili kuondokana na msongamano wa magari kwenye sehemu moja na mengine kukosa sehemu ya kuegesha.

Aidha amesema tiketi za kuingia katika viwanja vya maonesho zitakuwa zinapatikana pia katika vituo maalumu vya Mabasi yaendayo kwa haraka ili kuondokana na usumbufu wa kupanga foleni kusubiri tiketi katika maeneo ya Maonesho.

Sambamba na hayo amesema katika maonesho ya mwaka huu wamejipanga kuboresha huduma zao ambapo kutakua na huduma ya bure ya internet (Free Public Wife) katika Maonesho hayo yanayotarajiwa kuanza June 28, 2022.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI