Header Ads Widget

OJADACT YAWANOA WAANDISHI JUU YA MATUKIZI YA DAWA ZA KULEVYA

Na Matukio DaimaAPP,Mwanza 

Chama Cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT )kwa kushirikiana na ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza imeadhimisha siku ya kupiga vita dawa za kulevya na usafirishaji haramu wa binadamu kwa kuwahimiza waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuielimisha jamii athari za dawa za kulevya.


Mgeni rasmi ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Mwanza Daktari Thomas Rutachunzibwa alisisitiza waandishi wa habari kuwa daraja la kuelimisha jamii juu ya athari za dawa.



Dokta Rutachunzibwa pia ameishukuru OJADACT kwa kuandaa maadhikisho hayo kwa kuwaleta waandishi pamoja na kuwapitisha kwenye kujifunza athari za dawa za kulevya  na kusema kitendo cha OJADCT kuwepo Mwanza kunasaidia kwenye mapambano ya dawa za kulevya.


Mwenyekiti wa OJADACT Bwana Edwin Soko alisema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni tukubaliane na dawa za kulevya kwa ustawi wa jamii itumike kwenye kuielimisha jamii juu ya athari za dawa za kulevya Nchini.


Pia mtoa mada Daktari Eunice Masangu  alisema kuwa, kwa sasa hospitali ya Mkoa ya Sekeouture inatoa huduma ya methadone kwa watumiaji wa dawa za kulevya za iroine kwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa.


OJADACT inajikita kwenye mapambano ya dawa za kulevya Nchini hivyo kila mwaka inaadhimisha  siku hiyo.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI