Header Ads Widget

MBUNGE CHUMI AFANYA KONGAMANO KUBWA LA KUMPONGEZA RAIS SAMIA

 





NA RAYMOND MINJA MUFINDI


Mbunge wa Mafinga mji Cosato Chumi amefanya kongamano kubwa la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani kwa kupeleka miradi ya Maendeleo katika Jimbo Hilo.


Kongamano Hilo lenye lengo la kumpongeza Rais na kuainisha miradi mbalimbali  iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa kwenye Jimbo hilo lilifanyika Jana hukuu likichagizwa na maandamano  yaliyozunguka mjii wa mafingaa.


Akizungumza katika kungamano Hilo Chumi alisema kuwa Jimbo la Mafinga mji ni moja Kati ya majimbo yaliyopokea miradi mingi na mizuri hivyo hawana budi kumshukuru mama(Rais ) kwa miradi waliyowaletea.




Alisema moja ya changamoto iliyokuwa ikakabili  Jimbo Hilo ni pamoja na tatizo la maji lakini kwa Sasa linakwenda Kuisha kabisa kwani wamepata mradi mkubwa wa maji na unaenda kumaliza kilio Cha watu wengii.


"Jamani nyiee ni mashaahidi tulikuwa na shida ya maji lakini Sasa mi nimepata mradi na mradii huu ni mkubwa na ni kwa Mara ya kwanza tunaenda kuchuimbiwa visima vya maji na mabomba kutandikwa moja kwa moja bila ya kusubiri sijuii kipindii kinginee sisi mradi unakwenda kukamilika moja kwa moja  nani Kama mama?".


Chumi alisema kuwa Jambo lingine ambal0 lilikuwa inawaumiza kichwa ni swala la mbolea kuwa juu lakini walipoenda bungeni walienda kujenga hoja na serekali ikaamuoa kutoa VAT kwenye mbolea ili kumpunguzia mzigo mkulimaa.


"Kuna siku moja niko kwenye mkutano akaja mamaa mmoja na kunishika koti na kuniambia hembu niambiee babaa,niuzee madebee mangapi ya mahindi  ili niweze kupata mbolea hata mfuko mmoja,lile Jambo liliniuma Sana ndio mana Leo beii imepungua"


" Ngoja niwambie kitu ndugu zangu unajua Kazi ya mbunge sio kwenda kuizodoa serekali bungeni  Bali ni kuchukua maoni na changamoto zinazogusa maisha ya watu wako na kwenda kujenga hoja bungeni ili kuweza kupata ufumbuzi na mwarubaini wa changamoto za watu wako "


Cosato Chumi alisema kuwa Jambo lingine liliokuwa likipasua kichwa na kuwaumiza watu wa mafinga mji na majirani zao ni swala la kusikia Serekali itaangza kuagiza na  kununua nguzo kutoka njee ya nchi na kuachana na nguzo zinazozalishwa hapa nchini Jambo ambalo lilimfanya wafanyabiashara wa nguzo kuchanga nganyikiwa.


Alisema kuwa Hilo ni bomo ambalo lilikuwa linetengenezwa na Kuna baadhii ya watu walitaka kucheza mchezo ambao sio mzuri wa kuagiza nguzo njee na kuacha nguzo za ndani ya nchii Jambo ambalo lilikuwa linakwenda kuuwa uchumi wa watu wengi.



"Mimi kwa Moyo wa dhati kabisa nimpongeze waziri wa Nishati na madini Januari Makamba (shemeji yangu)kwa kusitisha zoezi la uagizaji nguzo kutoka njee kwani Jambo Hilo lilikuwa likienda kuuwa uchumi wa watu wengi,hapa hatuna budi kumshukuru na kumpongeza mama lazima tusemee mama asante sana"



Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi Daudi Yasini alisema wao Kama watekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi wanajivunia Rais Samia Suluhu kwani wanawena kutembeaa kufua mbele kwani ilani waliyokuwa wakiinadi kipindi Cha kampeni za uchaguzi  imetekelezwa kwa kiasi kikubwa.


Alisema wao Kama wasimamia ilani wa wilaya hiyo wameona miradi mingi imejegwa na mingine inaendelea kujegwa ikiwamo barabara iliyosahaulika muda mrefu ya Mgololo ambayo tayari upembuzi yakinifu ushafanyika.


"Lengo kongamano hili ni  kumpongeza Rais watu Samia Suluhu  kwa kazi kubwa aliyofanya ,kwani kila mmoja ni shahidi kwa namna Raisi wetu alivyotuletea miradi mingi na mizuri katika wilaya yetu hatuna budi kumshukuru na kusema asante kwani moyo unayoshukuru ndio unaopokea"




Frida Kaaya ni katibu wa CCM wilaya ya Mufindi amempongeza mbungee Chumi  kwa kutimiza majukumu yake ipasavyo Jambo ambalo litafanya kurahisiaha kazi ya kuwanadi wagombea ubungee uchaguzi ujao kwani wanetimiza majukumu Yao ipasavyo


Hata hivyo Kaaya alimshukuru Rais Samia Suluhi kwa kuwaketeaa miradi mikubwa kwani amekuwa ni Raiss msikivu na mnyenyekevu anayejishusha na kusikiliza na kutatua matatizo ya watanzania.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI