Na Mapuli Misalaba, MatukioDaimaAPP Shinyanga
Makamu Mwenyekiti wa Alat Taifa mheshimiwa Sima Costantine Sima amewahimiza vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ili kuendelea kuimarisha umoja wa vijana Nchini.
Hayo ameyazungumza wakati akifungua kikao cha baraza la Umoja wa Vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga Sima amesema katika uchaguzi unaofanyika kwenye jumuiya ya vijana ndani ya chama cha mapinduzi CCM, vijana wananafasi kubwa ya kugombea nafasi za uongozi huku lengo likiwa ni kujenga Taifa la Tanzania.
Mheshimiwa Sima ambaye ni mstahiki meya wa jiji la Mwanza akiwa mgeni rasmi kwenye baraza hilo amewasisitiza vijana kutokatishwa tamaa na changamoto za kimaisha na kwamba wanapaswa kusimama imara katika misingi ya chama hicho.
Sima amewaomba madiwani wote kuwa mabalozi wazuri katika kuendelea kulinda kundi la vijana ili waweze kufikia ndoto zao katika umoja wao kupitia chama hicho cha CCM.
''Vijana wengi tumekuwa tukikatishwa tamaa zinapofika nyakati za uchaguzi kila kijana anayonafasi ya kufika sehemu yoyote anayotamani kufika najua wengi tunatembea na ndoto zetu ukitaka kufika mbali lazima ndoto yako uipitishe ukitaka kufanikiwa lazima ndoto yako iwe kubwa zaidi vijana katika kipindi hiki ambacho tunaenda kwenye uchaguzi shauku yangu kubwa kijana yeyote wa Shinyanga akajaribu nafasi ambayo kesho atakuja kuiona nafasi yenye manufaa kwake''. amesema Sima
Aidha Makamu Mwenyekiti wa Alat Taifa mheshimiwa Sima Costantine Sima ameahidi kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili katika umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Shinyanga ikiwemo changamoto ya ukosefu wa baadhi ya vifaa katika ujenzi wa nyumba za viongozi wa umoja huo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge amepongeza jitihada anazofanya Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani Shinyanga.
Shemahonge amesema Rais Samia ameendelea kutatua changamoto ambazo zilikuwa zikiwakabili wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya pamoja na miundombinu ya barabara ambapo amewaomba vijana na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kumuunga mkoa Rais Samia.
Mwenyekti huyo naye ametumia fursa hiyo kuwaomba vijana katika Mkoa wa Shinyanga kuchukua fomu za kugombea nafasi ya uongozi bila kusita kwa kuzingatia misingi na utaratibu wa chama cha mapinduzi CCM.
Awali akisoma taarifa fupi ya utekelezaji katibu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Raphael Nyandi emeeleza baadhi ya mafanikio katika jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja na kuongeza wananchama wapya wa umoja wa vijana kutoka chama cha mapinduzi.
''Tumefanya ziara kuangalia uhai wa jumuiya na utekelezaji wa ilani hasa maeneo ambayo yanahitaji utoaji wa mikopo kwa vijana tumefanikiwa kuingiza wanachama wapya wa umoja wa wa vijana kutoka chama cha mapinduzi kwa wingi kutoka mashuleni, vyuo na kwenye maeneo mbalimbali na mashina ya wakeleketwa tumefanikiwa kujenga nyumba ya watumishi wa umoja wa vijana Mkoa na Wilaya zote za Mkoa wa Shinyanga''.
''Tumefanikiwa kuwaunganisha vijana kupata mikopo kutoka kwenye asilimia 4 ya makusanyo ya Halmashauri ya ndani lakini pia kusimamia maeneo ya miradi na kupatiwa hati miliki''.
Katibu huyo Nyandi ametaja baadhi ya changamoto zinazowakabili kwenye jumuiya hiyo ikiwemo changamoto ya ukosefu wa fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa nyumba za viongozi.
''Lakini pamoja na mafanikio hayo makubwa tunazo changamoto kwanza ukosefu wa fedha kwa ajili ya kukamilisha majengo ya watendaji kutokana na viongozi''. amesema katibu Nyandi















0 Comments