BARAZA la Wakulima Taifa (ACT) limepongeza bajeti ya Kilimo ya shilingi bilioni 750 itainua kilimo cha mboga mboga na matunda ambacho kwa sasa kinaongoza kwa kusafirishwa nje ya nchi na kuliingizia Taifa pato kubwa.
Hayo yalisemwa Mjini Kibaha Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo Jitu Soni alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Soni alisema kuwa kilimo hicho kinaongoza kwa kuuzwa nje na ndani ya nchi na yanaingizia nchi zaidi ya trilioni tisa.
Alisema kuwa Mboga mboga na matunda yanaiingizia nchi fedha nyingi hata ukiunganisha mazao yote ya nafaka na mazao kama vile ya Korosho, mkonge, tumbaku na kahawa yote yakiunganishwa hayawezi kufikia mazao hayo ya mboga mboga na matunda.
Aidha alisema kuwa kilimo hicho mauzo yake ya nje ya nchi yana thamani ya dola milioni 780 za Kimarekani kwa mwaka.
Aliongeza kuwa serikali imesema itaweka nguvu kwenye kilimo ambapo wizara husika zinaweka mazingira mazuri ambapo wasafirishaji wa parachichi walikuwa na vikwazo 13 ambavyo vimeondolewa.
Aliongeza kuwa wa upande wa magari yaliyokuwa yanasafirisha mazao kwenda bandarini ili yasafirishwe nje ya nchi yalikuwa yanasimamishwa muda na kusababisha mazao kupoteza ubora wake na kulikuwa na vikwazo ambapo kwa sasa wataweka alama ya kijani kwa mazao yanayoharibika na yataingizwa bandarini bila kukaa kwenye foleni huku la vibali bado linafanyiwa kazi ili kupatikana kwa muda mfupi.
Kwa upande wake Meneja wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Kibaha Hildelitha Msita alisema kuwa wanaendelea na utafiti wa mbegu za mazao ya miwa, mihigo na viazi na zimeanza kuzalishwa Kibaha.
Msita alisema kuwa wataweka mashamba mengi kwa baadhi ya wakulima ili yatumike kama mashamba darasa hivyo wanapoletewa elimu kwenye shamba wayatunze ili kuwasaidia na wakulima wanaozunguka ili mbegu zifike ngazi ya Vijiji na Kata.






0 Comments