Mtendaji mkuu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ((Tanzania Forest Services (TFS)
Prof. Dos Santos Silayo akizungumza na viongozi mbali mbali wa wilaya ya Mufindi ,Kilombero ,Kilolo na Njombe jana wakati wa uzinduzi wa kongamano la mikakati ya kuthibiti majanga ya moto wilaya ya Mufindi Leo ,kongamano lililofanyika ukumbi wa CCM wilaya ya Mufindi
WAZIRI wa maliasili na utalii Dkt Pindi Chana amewataka watendaji wa kata ,vijiji na wenyeviti wa vijiji pamoja na madiwani katika mikoa ya Iringa , Njombe na Morogoro inayozunguka shamba la miti la Taifa la Sao Hill kushirikiana kupambana na majanga ya moto yanayojitokeza katika maeneo yao ili kuepusha hasala kubwa inayojitokeza kutokana na miti kuteketea kwa moto .Mwandishi Francis Godwin MatukioDaimaAPP
Waziri Dkt Pindi aliyasema hayo leo katika kongamano la mikakati ya kupambana na moto ndani ya wilaya ya Mufindi ,kuwa suala la udhibiti wa uchomaji moto ovyo ni moja kati ya maagizo 15 yaliyotolewa na waziri mkuu Kasim Majaliwa wakati alipokuwa akihutubia Taifa kupitia kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira duniani Juni 5 mwaka huu jijini Dodoma.
Hivyo alisema utekelezaji wa maagizo hayo unapaswa kufanyika kwa haraka zaidi na kila mmoja kuwajibika katika utekelezaji wake na kuwepo kwa mikakati kabambe ya kudhibiti majanga ya moto katika maeneo yote nchini yakiwemo yale yanayozunguka mashamba ya miti ya Taifa kama shamba la Sao Hill na mengine.
Waziri Dkt Pindi katika hotuba yake iliyosomwa na mtendaji mkuu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS )Prof Dos Santos Silayo alisema kuwa si vema viongozi wa serikali ya vijiji kuacha watu wakipoteza maisha kwa presha inayotokana na uchomaji moto miti yao kutokana na uzembe wa baadhi ya watu wachache .
Hivyo alisema kupitia kongamano hilo la mikakati ya kudhibitio uchomaji moto ovyo ni uhakika kasi ya uchomaji moto ovyo ndani ya maeneo yote yanayozunguka hifadhi za misitu na mashamba ya watu binafsi ndani ya mkoa wa Iringa , Njombe na Morogoro itaendelea kupungua kama si kumalizika kabisa .
Alisema kuwa serikali kupitia wakala wa huduma za misitu Tanzania imewekeza ardhi yenye jumla ya hekta 135,603 kwa ajili ya uhifadhi na upandaji wa miti katika shamba la sao Hill kuwa serikali imeweka mikakati ya kupanda miti kwa awamu kulingana na mipango iliyowekwa .
" Wananchi baada ya kuona maeneo ya shamba la Miti Sao Hill yako wazi wameanza kuvamia kwa shughuli za kilimo ,upandaji miti na maeneo mengine kuweka makazi ,kutokana na hilo serikali imeanza kutatua mgogoro huo kwa kuainisha wavamizi kwenye vijiji 12" ikumbukwe kuwa maeneo hayo yapo kwenye mipaka iliyopimwa ,hivyo hata ukivamia zile alama hazitoki jambo la msingi ni wananchi kuacha kuvamia maeneo hayo" alisema waziri Dkt Chana
Kwa kwa mujibu wa taarifa za awali ya tathimini na utambuzi wa maeneo yaliyovamiwa ilithibitisha kuwa jumla ya Hekta 3,617.7 zimevamiwa wakati jumla ya wavamizi 962 waliweza kutambuliwa kwenye vijiji ambavyo vilikubali kufanyiwa tathimini na utambuzi wa maeneo yaliyovamiwa katika Hifadhi za misitu zinazopakana na vijiji hivyo .
Alisema kwa ujumla takwimu za aina ya uvamizi ilikuwa ni makazi asilimia 17 ,kilimo asilimia 16 na upandaji miti ya biashara asilimia 67 kwa sasa vijiji vya kibengu na usokami havijafanyiwa tathimini kwa sababu ya wananchi hawajajitokeza kufanyiwa tathimini hiyo.
Alisema serikali itaendelea kulinda eneo lake kulingana na mipaka iliyopo kisheria hivyo kuwaomba wenyeviti wa maeneo hayo yanayozunguka maeneo ya shamba la Sao Hill na maeneo yote ya hifadhi kusaidiana kutoa elimu kwa wananchi ili pasiwe na uvamizi .
Aidha alisema hivi karibuni suala la wizi wa miti limeanza kujitokeza kwa watu kuvuna miti ya makampuni ,watu binafsi na taasisi mbali mbali katika wilaya ya Mufindi kitendo cha kuiba miti mashambani kinarudisha nyuma maendeleo kwa waliopanda na kutunza miti hiyo.
Pia alisema wizi huo unawakatisha tamaa wadau wa miti lakini bado kuna maswali ya kujiuliza kwanini wizi wa miti unatokea sasa na jibu lake ni moja kuwa thamani ya miti imeongezeka hivyo jitihada za uhamasishaji wananchi upandaji miti katka ardhi zao unajitajika kuendelea zaidi ndani ya mkoa wa Iringa na Njombe pamoja na mikoa mingine ambayo hali ya hewa inaruhusu kilimo cha miti.
Awali mkuu wa wilaya ya Mufindi Saad Mtambule akimkaribisha mgeni rasmi alisema kuwa wilaya ya Mufindi imeweka mikakati mbali mbali ya kupambana na majanga ya moto na moja kati ya mikakati yake ni kufanya kongamano hilo la wadau wa sekta ya misitu ili kujiandaa kupambana na majanga ya moto pindi yanapojitokeza .
Kwa upande wake meneja mkuu wa kampuni ya Green Resources Ltd ( GRL) Hampus Hamilton alisema kuwa tathimini ya kampuni yake imebaini kubwa miti yenye thamani ya shilingi biloini 10 ambayo ni miti ya makampuni ,taasisi na watu binafsi pamoja na shamba la Miti Sao Hill imeteketea kwa moto kwa kipindi cha mwaka mmoja pekee .





0 Comments