Header Ads Widget

"WAZAZI WAAMBIENI UKWELI WATOTO WENU"_VICTOR



TITUS MWOMBEKI- Muleba.


Wazazi na walezi wilayani Muleba mkoani Kagera  wametakiwa kuwaambia ukweli watoto wao ili kuelewa mabadiliko ya miili yao.


Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa shilika lisilo la kiserikali HUMULIZA Victor Nestory katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima, huku akiliitupia macho suala la utandawazi kuchangia katika mabadiliko hayo.


"Mabadiliko ya utandawazi Katika jamii yanaendana sambamba na mabadiriko ya mwili kwa watoto hivyo wazazi tuwe wawazi ili wajue kinacho endelea kwa watoto wetu"


Hata hivyo Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa, jamii imezipuuza Mila na desturi kwa asilimia kubwa watu wako bize na Maisha kuliko kuwajali watoto wao, huku wakiwatupia mizigo walimu mashuleni kubeba 


Mkurugenzi huyo amesema kuwa, shirika la Humuliza limeweka malengo ya kuwafikia watoto 2600 kila mwaka kwa zaidi ya miaka mitano (5) pamoja na kutoa  msaada wa kisaikorojia kwa  watoto ambao wamekuwa wakipatwa na changamoto  mbalimbali ikiwamo ukatili pamoja na mimba za utotoni.


Kwa upande wake Meneja Mradi Lightess Mpunga wa shirika la HUMULIZA, amesema kuwa asilimia kubwa watoto wapo kwenye mazingira hatarishi kuanzia Shuleni na hata nyumbani.


" Napata shida Sana kulizungumzia hili kwani watoto wapo Katika mazingira hatarishi maana ndani unamkuta wazazi au walezi awashiriki kikamilifu katika  malezi ya watoto hawa,  jamii ibadilike kwani tatizo kubwa sana linapomkumba mtoto inakuwa ngumu kwao kusema kuwa nimefanyiwa ukatili" amesema.


Ameeleza kuwa ,katika kipindi cha mwaka 2021 yamelipotiwa matukio 74 yanayo usishwa na watoto ambao wamefanyiwa ukatili wa aina Mbalimbali hapa nchi huku waanga wakubwa wakiwa ni watoto wakike.


Sambamba na hilo, awaomba wazazi kuepuka kuwalaza chumba kimoja  watoto wao  pamoja na wanaowatembelea ili kuwalinda watoto hao kwani dunia imebadilika Sana.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI