Na Gabriel Kilamlya NJOMBE
Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Kutangaza Ongezeko la Mshahara kwa Watumishi wa Umma Kwa Asilimia 23.3 Kima Cha Chini Baadhi ya Watumishi Mkoani Njombe Wamepongeza Uamuzi Huo Wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa.
Miongoni Mwa Watumishi Hao ni Pamoja na Katibu wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya[TUGHE] Angel Chipindula ambaye Amesema Hawakutarajia Kama Ahadi ya Rais Ingetekelezwa Mapema Hivyo Tangu Atoe Ahadi Yake Hapo Mei Mosi ya Mwaka Huu.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Waziri Waziri Kindamba Anasema Serikali ya Mkoa wa Njombe na Watumishi Wake Wanashukuru Sana Kwa Utekelezaji wa Ahadi Hiyo ya Rais na Kwamba Kazi Iendelee.
Wilbard Mwinuka ni Diwani wa Kata ya Luana Wilayani Ludewa Ambaye Licha ya Wao Kama Madiwani Kutohusika Katika Kiwango Hicho Cha Mshahara Lakini Amepongeza Hatua Hiyo Kwa Kuwa Inawaongezea Urahisi wa Kuwasimamia Watumishi Huku Akiomba Nao Waangaliwe Kwenye Posho Zao.
Kwa Upande Wake Katibu wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa TALGWU Mkoa wa Njombe Raymond Chimbuya Amesema Watumishi Hivi Sasa Wamepata Matumaini Makubwa.
Mei Mosi ya Mwaka Huu Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Aliwaahidi Watumishi Kwenda Kuwaongezea Watumishi mshahara na sasa ametekeleza.
0 Comments