Header Ads Widget

PSPTB YAWATAKA WAAJIRI KUWAONDOA MAAFISA WASIO NA SIFA

 


Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam



Bodi ya wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imewataka waajiri wote nchini Tanzania kuwaondoa kwenye kitengo cha ununuzi na ugavi maafisa wote wasio na sifa za kitaalam kwa mujibu wa muongozo wa usajili.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Godfred Mbanyi amesema kuwa waajiri wote wanatakiwa kuajiri watu wenye sifa kwa kufuata muundo wa utumishi wa kada zilizopo chini ya Wizara ya fedha na Mipango, waraka No.3 wa mwaka 2015.


Amesema kuwa, waraka huo wa utumishi wa kada zilizopo chini ya Wizara ya fedha No.3 wa mwaka 2015 umeanisha nafasi mbalimbali za ngazi za ukuaji za fani ya ugavi na ununuzi hivyo, watu wapangiwe majuku yao kupitia muongozo huo.


Aidha, PSPTB inaawagiza wataalamu wa ununuzi na ugavi wa Sekta binafsi na umma kufanya kazi kwa weledi na kutoa ushauri kwa umakini bila hofu Ili kupata Thamani ya fedha.


Hata hivyo, amewataka wataalamu wote wanaofanya kazi kwenye kitengo cha ununuzi na ugavi kuhakikisha wanafanya kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao kwa mujibu wa  PSPTB code of Ethics and Conduct GN.365/2009 inayowataka wataalamu kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliyopoili kutoa huduma yenye kukidhi viwango.


Aidha, amesema kupitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Mamlaka ya kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) zimeonyesha ukiukwaji mkubwa wa sheria kwa kitengo cha ununuzi kuwa na wakuu wa vitengo wasio na sifa za kitaalam.


Ameongeza kuwa, pia taarifa hiyo imebaini mapungufu makubwa kwenye kukidhi sheria ya ununuzi wa Umma na kanuni zake na kupelekea hasara kwa Serikali.


Hata hivyo, amesema kwa mujibu wa kifungu cha 11 cha sheria ya PSPTB kimeweka sharti la ulazima kwa kila anaefanya kazi za ugavi na ununuzi awe amesajiliwa na PSPTB, ambapo kifungu cha 46 kinazuia kuajiri au kufanya kazi za ununuzi na ugavi kwa mtu yoyote ambae ambae hajasajiliwa na bodi hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI