Header Ads Widget

HALI YA UTOAJI CHANJO NCHINI YAENDELEA KUIMARIKA

 



Kwa kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022, Wizara ya Afya ilihakikisha chanjo na vifaa vya kutolea chanjo vinapatikana kulingana na mahitaji ya Mikoa yote nchini.


Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo Mei 16,2022 kwenye hotuba yake ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2022/2023 Bungeni jijini Dodoma. 


"Lengo likiwa ni kuhakikisha Kuwa watoto 2,061,343 wenye umri wa chini ya mwaka mmoja, wajawazito 2,229,015 na Wasichana 685,580 wenye umri wa miaka 14 ambao ni walengwa wa huduma za chanjo kwa mwaka 2021/22 wanapata huduma za chanjo kwa wakati." Amesema Waziri Ummy 


Hadi kufikia Machi 2022, hali ya utoaji wa chanjo nchini imeendelea kuimarika, ambapo chanjo kwa Watoto wa chini ya umri wa mwaka mmoja kwa chanjo ya Penta kwa ajili ya kuzuia magonjwa ya Dondakoo, Kifaduro, Kupooza, homa ya ini na homa ya uti wa mgongo ambayo hutumika kama kipimo kikuu cha Shirika la Afya Duniani (WHO).

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI