Header Ads Widget

WATOTO ZAIDI YA 103O ELFU WA KAYA NUFAIKA MUFINDI WAGAIWA TAULO ZA KIKE

 

Watoto zaidi ya elfu moja Mia tatu kunufaika na mradi wa tasafu kwa kutoa taulo za kike kwa walegwa  wilayani Mufindi

NA RAYMOND MINJA MATUKIO DAIMAAPP , IRINGA 

Jumla ya Watoto 1037  wanufaika wa kaya Masikini wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa wamegaiwa taulo za kike kwa ajili ya kujisitili  ili waweze kubaki shuleni na kuhudhuria vizuri  masomo yao bila vikwazo vyovyote.


Akizungumza hii leo mei 7,2022 Mwezeshaji wa TASAF wilayani hapa, Abduli  Chile amesema kuwa  mradi huo umelenga kuwasaidia jumla ya watoto  wa kike  1037 wa shule ya msingi na Sekondari  wenye umri wa kati ya miaka 11 hadi 18.


"TASAF  kushirikiana na UNICEF ambao ndio  wafadhi kuona kwa sasa umri wa watoto hao miaka 11 hadi 18 wakuwa wanaweza kutumia taulo hizi za kike ndio maana wakaandaa mpango huu wa taulo za kike  kuwagaia watoto wa wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini." Amesema Chile.


Amesema wameamua kupita mashuleni kutekeleza mradi huo kuwagaia  taulo za kike kwa sababu walengwa  wengi bado wapo shule na inakuwa rahisi kuwafikia watoto wenyewe na kuwakabidhi kwa sababu ndio ambao wamelengwa kupewa na siowazazi.


Kwa upande wake Mwalimu wa shule ya Msingi Ihegela  Hawa Mwanga alisema  wanafunzi wengi walikuwa wanashindwa kuhudhulia vizuri masomo yao darasani kutokana na kukosa kwa taulo za kike kwa ajili ya kujisitiri hali ambayo ilikuwa ikiwalazimu kukaa nyumbani Siku 2 hadi 3 bila kufika shule.


" tunashukuru sana TASAF kwa kushirikiana na UNICEF kugawa taulo za kike  kwa sababu utasaidia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa utoro kwa wanafunzi wa kike kutokana na watoto wataweza kuhudhuria masomo yao baada ya kupatiwa vifaa hivyo vya kijisitili( Taulo za Kike). Amesema Mwanga


Aidha Mwalimu huyo amewashuri wanafunzi hao kuhudhuria masomo yao ipasavyo kutokana na kwa sasa wamepatiwa vifaa hivyo vya kujisitili au Taulo za kike ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.


Naye mmoja wa mwanafunzi ambaye amenufaika na kupatiwa taulo hizo za kike Diana Ngaemba ameishukuru UNICEF kupitia TASAF kwa msaada huo ambao wamewapatia kwani itawasaidia kuhudhuria vizuri masomo yao shule tofauti na kipindi cha nyuma.


"Kipindi cha nyuma tikuwa tunashindwa kuhudhuria masomo yetu vizuri kutokana na kukosa taulo hizi za kike hali hivyo ili kuwa ikitufanya tujisikie vibaya lakini kwa sasa tumepewa taulo hizi kupitia Tasaf kwa kushirikiana na UNICEF  hivyo  itatusaidia kufanya vizuri katika masomo." Amesema Ngapemba


 Naye Yunis mhema  alisema msadaa huo utawaasaidia Sana kwani wakati mwingine walikuwa wakitoroka shule ili kwenda kujisiriri nyumbani,


"Mi niishukuru sana serekali kupitia tafafu kwa huu msada waliitupatia kupitia shirika ka kusaidia watoto UNCF  kwa msadaa huu kwakweli wamatusaidia Sana sisi watoto"


Hata hivyo mhema aliomba serekali kuangalia namna ya kuwasilisha fedha za watoto wenye uhitaji shuleni kwani baadhii ya wazazi wakishapokea fedha hizo za tasaf huwa wahasahuu kuawanunulia watoto wao mahitaji muhimu ya shule ili Hali ni Jambo la msingi na nimeelekezwa kwenyee maagizo ya TASAF

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI