Header Ads Widget

WAKULIMA WA MUHOGO NAMTUMBO WAOMBA KUONGEZEWA MBEGU

 

 


Na Mwandishi wetu, Namtumbo


Wakulima wa zao la muhogo wilayani Namtumbo wameomba kuongezewa mbegu za muhogo ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo katika Wilaya  hiyo. 


Akizungumza na watafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari-Naliendele) Afisa Kilimo Wilaya ya Namtumbo Andrew Tarimo alisema kuwa wakulima wengi wamehamasika kulima zao hilo lakini wanakabiliwa na changamoto ya mbegu. 


Alisema kuwa endapo mbegu zitapatikana kwa wingi  watahakikisha kuwa wakulima wanazalisha kwa tija kwakuwa wamepata mafunzo na wameweza kuona mbegu zipi zinafaa kulima katika eneo lao. 


“Mwanzo kilimo walikuwa wanalima wanavuna kisha wanatafuta soko lakini sasa wakulima wanaanzia sokoni ili kujua mahitaji kisha tunalima kwakufuata vigezo na mahitaji ya soko ujio wa mbegu zinaokomaa ndani ya mwaka mmoja kwa mkulima ni fursa kubwa” alisema Tarimo


Nae Juma mchatta mkulima wa kitongoji cha ushirika  alisema kuwa kitendo cha kupata elimu hiyo kimewapa fursa kubwa ya kuweza kuliangalia tena zao la muhogo. 


“Sisi hatukujua faida za mbegu wala za kulima zao la muhogo tulishaacha lakini kupitia mbegu bora itatuhamasaisha zaidi na kutupa molali ya kulima kwkauwa tunaamini tutapata faida kibiashara na kutukuza kiuchumi hili zao kwetu  ni nyongeza ya zao la biashara zamani tulikuwa tunalima muhogo tule tu nyumbani lakini sas tutafanya biashara”  alisema Mchatta


Nae Edward Haule mhamasishaji wa zao la muhogo wilayani Namtumbo(mchechemuzi) alisema watanzania ni vema wakarejea kuanza kulima zao muhogo kwakuwa ndio zao pekee ambalo lilikuwa msaada mkubwa nyakati za njaa. 


“Zamani muhogo ulikuwa ni kinga ya njaa lakini leo tunahamasishawa kulima kama kilimo biashara hali ambayo inapelekea wakulima kuelekezwa ili kuweza kuzalisha kwa tija iili waweze kupata mazao yenye tija tena zinastahimili magonjwa na kulizalisha mazao mengi katika eneo dogo” alisema Haule 


Kwa upande wake Afisa kilimo kutoka taasisi ya utafiti wa Kilimo Tari  Naliendele Florah Liyumba alisema kuwa uvunaji wa mbegu hizo ulijumuisha wakulima ili kuwapa fursa ya kuona mbegu gani inafaa katika eneo lao. 


“Tumekuja kuvuna mbegu za zao la muhogo na kuwaonyesha wakulima ubora wake na kuwapa nafasi ya kuchagua ipi itawafaa katika shamba darasa ili kuweza kuhamasisha wakulima kulima mbegu bora ambazo ni kinzani kwa magonjwa ya michirizi, kahawia na batobato”  alisema Liyumba 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI