Header Ads Widget

WAKULIMA WA MIHOGO TUNDURU WAIPONGEZA TARI

  

Na Matukio Daima APP ,Tunduru

Wakulima wa kijiji cha Chingulungulu Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wameipongeza Wizara ya Kilimo kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Tari Kituo cha Nalindele kwakuwaletea mbegu bora ya Muhogo.

Wakizungumza mara baada ya kuvuna zao la muhogo na kushuhudia mavuno mengi katika eneo dogo Hadija Ally mkazi wa kijiji hicho alisema kuwa mbegu hizo zimeenda kuwapa hamasa zaidi ya kulima zao hilo.

 “Yaani hii ni mihogo bora ambayo imekuwa ikitupa hamasa ya kulima kwakuwa tunapata mihogo mingi ambayo tukiuza tunaweza kuboresha maisha yetu”

Nae Said Issa mkazi wa kitongiji cha Temeke alisema kuwa Ipo tofauti kubwa kati ya mbegu ya asili na mbegu bora iliyofanyiwa Utafiti na Watafiti wa TARI Naliendele. 

“Nilipokuta mihogo imechimbwa nilishangaa kwakuwa eneo ni dogo lakini tumepata mihogo mingi wakati zamani ili upate mazao kama hayo unalazimika kulima heka nzima hii ni mbegu bora kwetu” 

Nae Mwenyekiti wa kitongoji cha Temeke kata ya Muhesi Wilayani Tunduru Chande alikaweje  alisma kuwa elimu hiyo imeenda kuongeza hali na hamasa ya kulima zao la muhogo. 

“Zamani tulikuwa tunatumia mbegu ambayo haikuwa na mavuno mengi pia ilikuwa na magonjwa mengi hivyo kutufanya tulime kwa mazoea lakini ujio wa mbegu hizi za kitaalamu kwetu zitaleta tija zaidi sokoni na chakula pia” alisema Chande  

Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Wilaya ya Tunduru Morton Msowoya alisema kuwa wakulima wanapaswa kuzingatia ushauri wa watafiti hao. 

“Ni muhimu kuwa na vikundi vya uzalishaji wa mbegu za muhogo ili waweze kuwa na ufahamu zaidi na kuzalisha kwa wingi zao la muhogo lakini pia tunafanyakazi kubwa na TARI naliendele wamekuwa na mchango mkubwa katika mazao mbalimbali nchini” alisema Msowoyo

Kwa upande wake Mtafiti wa Zao la Muhogo kutoka Tari Kituo cha Naliendele Festo Masisila alisema kuwa katika kijiji hicho walifanikiwa kupanda mbegu aina 11 katika shamba darasa. 

“Tuligundua kuwa maeneoe haya uzalishaji haukuwa wa tija kwkauwa hawatumii mbegu bora ambazo zinavumilia magonjwa batobato na michirizi kahawia  lakini zinavumilia ukame ikawa fursa tumewaletea na tumevuna pamoja zikiwemo aina za Mkuranga, pwani, kizimbani, kipusa, tarikasi kuanzia 1-5” alisema Masisila 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI