Header Ads Widget

WAHAMIAJI HARAMU 69 WAFIKISHWA MAHAKAMANI.

 




WAHAMIAJI  haramu 69 kutoka nchini Ethiopia wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Mwanza wakikabiliwa na kosa la kuingia na kuishi nchini bila kibali.


Kadhalika, Takila Mlawa ambaye ni Mtanzania amefikishwa katika mahakama hiyo kwa kosa la kupanga na kusaidia kusafirisha wahamiaji hao kinyume cha sheria za uhamiaji.


Washtakiwa hao kwa pamoja walifikishwa juzi jioni katika mahakama hiyo na kusomewa mashtaka mawili mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, Bonaventure Lema.


Wakili wa serikali kutoka Idara ya Uhamiaji mkoani Mwanza, Patrik Ngayomela aliimbia mahakama hiyo kwamba Aprili 29, mwaka huu katika eneo la Usagara wilayani Misungwi mkoani Mwanza, wahamiaji hao walikamatwa wakiwa wamehifadhiwa nyumbani kwa mtu.



Alisema idara ya uhamiaji kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama waliwakamata wahamiaji hao pamoja na Mtanzania mmoja wakiwa katika nyumba hiyo.


Alidai mahakamani hapo kwamba raia hao wa Ethiopia hawakuwa na kibali chochote cha kuwaruhusu kuingia nchini na kuishi.


Hata hivyo, kesi hiyo ilishindwa kuendelea kutokana kukosekana kwa mkalimani wa lugha ya wahamiaji hao.


Katika shtaka la pili ambalo linamkabili mshtakiwa namba moja, Talika Mlawa, Wakili huyo wa serikali alisema anakabiliwa na kosa la kupanga  njama za kusaidia kusaidia wahamiaji hao.



Mshtakiwa namba moja alipewa dhamana na kuwa nje huku wahamiaji hao wakikosa wadhamini licha ya kuwa kosa lao lina linadhaminika.


 Hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 19, mwaka huu ikapofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI