Header Ads Widget

WADAU WA UTALII WAMETAKIWA KUTUMIA FURSA YA MIKOPO KATIKA KUIMARISHA VIVUTIO VYA UTALII NCHINI.




Teddy Kilanga _Arusha



Katibu mkuu wa wizara ya maliasili na Utalii,Dkt Francis Michael amewataka wadau wa utalii mkoani Arusha kutumia fursa za mikopo nafuu ya Taasisi ya fedha(NMB) katika kuwekeza katika sekta ya utalii ili kuvutia wageni nchini.



Akizungumza katika kongamano mitandao ya utalii(tourism Networking)Dkt.Michael alisema benki ya NMB imekuwa chachu katika kuhakikisha inawapa mikopo wadau wa sekta ya utalii katika kuhimarisha mazingira ya vivutio nchini.


"Tunaomba mfanye jitihada za kuijenga sekta ya utalii kwani serikali imeshaweka mazingira ya kuitangaza kupitia filamu ya Royal tour ambao hadi sasa kuna baadhi ya hoteli zimeshajaa wageni hivyo ni kitu cha kujivunia kwetu na nyie kama wadau ni vyema mkatumia fursa hiyo katika kuweka mazingira sawa,"alisema Dkt.Michael.


Aidha aliwasisitiza wadau hao kutumia benki ya NMB katika kuhimarisha ulinzi na usalama wa watalii ikiwemo vituo vya polisi hivyo ni vyema wadau hao wakaongeza juhudi katika kuongeza idadi ya wageni nchini pamoja na kuwahudumia ipasavyo.


Naye Mbunge wa jimbo la Arusha mjini,Mrisho Gambo alimshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuzindua filamu hiyo iliyoleta matokeo chanya kwa muda mfupi lakini ni vyema NMB ikaongeza muda wa nyogeza kwa wateja wao waliokopa katika kipindi cha mlipuko wa ugonjwa wa covid 19 kuwaongezea muda marejeshi  pasipokuwa na riba.



Kwa upande wake Afisa mkuu wa biashara na wateja binafsi wa NMB Filbert Mponzi alisema benki hiyo wanaendelea  kuunga juhudi  za serikali ya awamu ya sita kupitia Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania,Rais Samia Suluhu Hassan.



Pia alisema uhitaji wa watalii wengi nchi imeongeza chachu katika kujiandaa kupitia Taasisi ya benki ya NMB kwa kuunga mkono watoa huduma katika sekta ya utalii kwa lengo la kuongeza ufanisi zaidi katika kuwapokea watalii nchini.


Mponzi alisema kuwa kwa miaka ya hivi karibuni tumeanza  kutoa huduma ya mikopo katika sekta ya utalii lengo ni kuhimarisha katika kutoa huduma kwa wageni wanaofika nchini kutalii na kuona vivutio vilivyopo nchini.


"Bado tunaendelea kutoa katika sekta ya utalii kwa lengo la kufanya vizuri zaidi na sasa tumejipanga kuwahudumia wageni wote wanaofika nchini,"alisema  Afisa huyo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI