Header Ads Widget

WADAU WA ELIMU WACHANGIA TAULO ZA KIKE SHULE 18 NJOMBE

 


NaNa Gabriel Kilamlya NJOMBE


Ili Kuokoa Siku Takribani 36 za Wanafunzi wa Kike Kukosa Masomo Kutokana na Kukosa Taulo za Kike kwa ajili ya Kujisitiri wakati wa Hedhi Wadau Mbalimbali wa Elimu Wamelazimika Kuunga Mkono Jitihada za Serikali Kwa Kuwanunulia Taulo Hizo wanafunzi wa Shule 18 za Mkoa wa Njombe.


Wadau Hao Wa  Elimu Ikiwemo Kampuni ya Mtewele General Traders ya Mkoani Njombe Kwa Kushirikiana na Kampuni ya Rosper International Company Limited ya Nchini Japan Zimelazimika Kutumia Zaidi ya Shilingi Milioni 83 kununulia Taulo Hizo Boksi 2600 kwa ajili ya Kuwasitiri Wanafunzi Hao.


Katika Zoezi la Ugawaji Taulo Hizo Lililofanyika Katika Shule ya Sekondari Mpechi Mjini Njombe Kwa Niaba ya Shule 18 za Mkoa wa Njombe Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mtewele General Traders Bwana Sady Mwang'onda Anasema Hatua Hiyo ni Moja ya Kurudisha Fadhila Kwa Jamii Kutokana na Biashara Mbalimbali zikiwemo za Usambazaji wa Pembejeo za Kilimo Wanazozifanya.


Kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Njombe Afisa Tarafa Njombe Mjini Lilian Nyemele Amesema Kupatikana kwa Taulo Hizo Kunapaswa Kuwafanya Wanafunzi Kuongeza Juhudi Katika Masomo Kwa Kuwa Changamoto ya Hedhi Inapungua.


Lusiana Mgani na Asunter Mwesongo ni Baadhi ya Wanafunzi wa Kike Waliopatiwa Msaada Huo Ambao Wanakiri Kuwa Changamoto za Maisha Zimekuwa Zikiwasababisha Baadhi yao Kukosa Masomo Kutokana na Kukosa Fedha za Kununulia Taulo Hizo.


Mwalimu wa Afya Katika Shule ya Sekondari Mpechi Christa Chawe na Agusta Wella Mwakilishi wa Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Mji wa Njombe Wanapongeza Hatua ya Makampuni Hayo Kuwakumbuka Wanafunzi Huku Wakiweka Wazi Changamoto za Kukosekana Kwa Taulo za Kike Kwa Wanafunzi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI