Header Ads Widget

"NAAGIZA POSHO ZA WENYEVITI NA WAJUMBE KUANZA KULIPWA JULAI 2022 "_WAZIRI KINDAMBA

 


Na Frederick Siwale -Mdtv Makambako Njombe.                             

Mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba ameagiza  posho zilizoondolewa kwa Wenyeviti na Wajumbe wa Serikali za mitaa na Vijiji katika Halmashauri ya Mji Njombe zianze kutolewa na kulipwa katika muda wa mwaka wa fedha wa Serikali mwezi Julai.    


Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Bw.Waziri Kindamba wakati akizungumza na Wenyeviti,Watendaji wa Serikali za mitaa na Vijiji pamoja na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi  ( CCM) Wilaya ya Njombe katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Makambako.                



"Kuna mambo yanaonekana kukwama kutokana na kumegeka au kukatika kwa mnyololo kati ya Watendaji ngazi ya Halmashauri na Viongozi wa Mitaa na Vijiji ambao ndiyo Watendaji na walio karibu na Wananchi jambo ambalo ni hatari kwa mstaakabari  wa kujiletea Maendeleo kwa Wananchi." Alisema Mkuu wa Mkoa wa Njombe.              


 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako nafahamu wewe ni mgeni umefika hapa ukakuta pako hovyo hovyo fanya maboresho anza mwaka wa fedha Julai kuwalipa posho hawa Viongozi wa Mitaa na Vijiji ili kuleta ufanisi wa kazi.                                          


"Haiwezekani mtu akusanye mapato kutoka katika eneo lake na akakuletea chote pasipo kupewa posho hii ni kumfanya  mtu huyo arudi nyuma kiutendaji na hasa katika kuhamasisha" Alisema Bw.Kindamba.                      



Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako Mh.Chesco Mfikwa aliomba  Mabalozi wa mashina ingaliwe namna ya kuanza kupewa posho ili kuongeza hamasha na kuchochea shughuli za maendeleo kwa Wananchi katika maeneo yao.                      


Mh.Hanana alisema Balozi ni mtu muhimu sana na ndiyo mwenye watu mwanzo kabisa na Balozi ni Kiongozi wa ngazi ya chini lakini ndiye mwenye watu na ndiye anayewafahamu mmoja mmoja na ndiye anayetumika kwa kila kitu lakini ndiye anayefanya kazi bila kupewa mshahara wala posho.                        


Alisema iangaliwe kupitia Chama ambacho ndicho chenye mabalozi na hata Serikali ijaribu kuliangalia jambo hili la kuwatumikisha hawa Mabalozi bila ya kulipwa posho.                   



Upande wake Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Njombe Komredi Hitra Msola alisema tatizo linalozorotesha shughuli za maendeleo za kujitolea ni tabia ya chuki na husudi za kuchukiana kwa kuuondoa Upendo kati ya mtu na mtu na Kiongozi na Kiongozi mwenzake .                       


Komredi Msola alisema dhambi hii pamoja na ile ya uongo ni changamoto kubwa sana hasa kwa Wanasiasa kulekea changuzi za ndani ya Chama watu wanakuwa hawapendani na kuomba tabia ya Upendo irudi kama alivyosisitiza Mkuu wa Mkoa kuwa Wana Makambako na Wananjombe tupendane kwa kuhimiza ushirikiano na Upendo kwa kila mmoja wetu.                    

..


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI