NA ANDREW CHALE, ZANZIBAR.
RAIS wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekata kiu ya Wafanyakazi kwa kuongeza nyongeza ya mishahara kwa kuzingatia ngazi ya elimu, uzoefu na ujuzi.
Akitangaza mapema leo Mei 8, katika viwanja Mahisara Mjini Unguja, Rais Mwinyi alisema kuwa, amepokea mapendekezo mbalimbali na ongezeko hilo litaanza kuanzia mwaka wa fedha ujao 2022/2023, ambapo Wafanyakazi nyongeza hiyo itatokana na elimu yake pamoja na uzoefu wake kazini.
''Nawapongeza kwa dhati viongozi wa Shirikisho ya vyama huru vya wafanyakazi Zanzibar, mmeandaa vyema sherehe hizi na zimefana sana.
Pia natoa pongezi kwa waajili sekta ya umma na sekta binafsi kwa kufanya kazi njema na ushikamano.'' Alieleza Rais Mwinyi,
Na kuongeza kuwa, hii ni siku ya kuongeza ufanisi na kukumbushana wajibu wa wafanyakazi katika kutekeleza wajibu wa wa kuchochea mambo mbalimbali, kwani siku hii ina nafasi kubwa kwa Serikali.
Rais Mwinyi amesema kuwa, anatambua wafanyakazi wanataka kusikia habari njema, hivyo ametoa nyongeza hiyo.
''Ndugu wafanyakazi, natambua kwamba nyote mnategemea kusikia habari njema.
Risala iliyosoma hapa, imetoa mapendekezo. Lakini kama kawaida, mambo yanategemea uwezo na uchumi wa nchi, kwa hivyo habari njema niliyokuwa nayo leo, ni kwamba kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kuanzia Julai, Serikali itaongeza mishahara kwa kutumia utaratibu wa kuwapanga watumishi kwenye madaraja na vyeo vya kiutumishi kwa kuzingatia elimu, uzoefu na ujuzi wa kazi zao.'' Alisema Rais Mwinyi,
Amesema ongezeko hilo litaboresha litakuwa na mchango kwa watumishi wa umma kujikimu kimaisha na uwezo na kiwango cha ufanisi.
Aambapo Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 12.7 kwa mwezi sawa na shilingi bilioni 153 kwa mwaka katika kugharamia kwenye ongezeko hilo la mishahara.
''Kutokana na utaratibu huu, mshahara wa kima cha chini kwa mtumishi mpya aliyeajiliwa mwaka 2019 utapanda kutoka shilingi 300,000 hadi shilingi 347,000, ikiwewa ni ongezeko la asilimia 15.6.
Vilevile kwa mtumishi wa elimu ngazi ya cheti katika masomo ya Sanaa, aliyeajiliwa mwaka huo huo, utapanda kutoka Shilingi 321,000 hadi 382,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 19, kila mfanyakazi atapata nyongeza hiyo kutokana na elimu yake pamoja na muda aliofanya kazi,
'huko nyuma, tulizoea kusikia tumepandisha kima cha chini, lakini wote wangekuwa wamepandishiwa hata yule mwenye ngazi ya cheti, ila kwa sasa yule aliyeko Serikalini zaidi ya miaka 10, wao watapata nyongeza zaidi, uenda kile walichosema viongozi wenu hapa''. Alisema Rais Mwinyi.
Rais Mwinyi alisema kuwa, kuna watu wamefanya kazi kwa miaka mingi kwa muda mrefu hao fedha zao zitapanda sana hata kama hawana vyeti.
Vilevile, alisema Serikali kupitia mfumo wa hifadhi ya jamii ZNSSF, wameanzisha mafao ya upotevu wa ajali, na mwaka ujao wataanza kutoa kwa walengwa.
Aidha, serikali imeanzisha bima ya afya kwa kila mfanyakazi, ambaoo lengo kuwa bima ya afya kwa kila Mzanzibari.
''Fao la upotevu wa ajali na fao la aliyeumia kazini, kwa sasa tunakamilisha taratibu za kisera, serikali itaendelea kuimalisha maslai ya watumishi wa umma, kadri mipango itakavyohusu.
Pia kuwa na bima ya afya kwa kila mzanzibar na pia mchakato wa kulipa madeni ya wafanyakazi, tayari Bilioni 1.8 imeshaanza kutolewa kwa wafanyakazi wote ikiwemo likizo ya uzazi, uhamisho, vifo na mengine' alisema Rais Mwinyi,
Ambapo kwa sasa amebainisha kuwa, zoezi la uwajibikaji kwa watumishi wa umma linaendelea na kupitia chuo cha watumishi wa umma wanaendelea kutoa kozi fupifupi.
Aidha, Serikali kwa kusaidia na wadau wa kimaendeleo wanaendelea kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma,
Kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023, wanatarajia kutoa ajira mpya 5639 katika sekta ya Elimu na Afya.
Hata hivyo, mwinyi amepongeza mifuko ya fedha kwa kuweza kutoa mafao kwa walengwa kwani ni wajibu na wa msingi kwa walengwa kupata stahiki zao.
Katika hali ya kupanda kwa gharama za kimaisha, amesema kuwa, uchumi wetu umepata mtikisiko ikiwemo mfumuko wa bei na ongezeko la bidhaa na huduma mbalimbali kwa baadhi ya bidhaa ambapo tayari wamepunguza tozo ikiwemo kwenye bidhaa za chakula ikiwemo Sukari,
''Tutaendeleza sekta ya kilimo, sekta ya utalii na sekta ya uvuvi, katika pia kukuza biashara.'' Alisema Rais Mwinyi.
Aidha, amewahimidha wananchi kuendelea kumfikishia kero kupitia mfumo wa sema na Rais, ambapo kero zote anazipitia na kuzitolea ufafanuzi.
Mwisho.
0 Comments