Header Ads Widget

MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI YA MAENDELEO MEI 12

 


Na Fatma Ally, MDTV Dar es Salaam


Mwenge wa Uhuru  unatarajia kuzindua miradi ya maendeleo iliyopo Wilaya ya Ilala, Jijini Dar es Salaam Mei 12 mwaka huu.


Akizungumza na Waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ndatwa Ludigija, amesema Mwenge wa Uhuru unatarajia kupokelewa Kinyerezi Mtaa Kifuru Jimbo la Segerea.


Ludigija amesema siku ya Mei 12 Mwenge utakapowasili Ilala unatajia kupokelewa saa kumi na mbili Asubuh Kata ya  Kinyerezi .


Aidha, amewataka Wananchi wa Wilaya ya Ilala kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Mwenge siku hiyo.



Hata hivyo, amesema  Mwenge huo mara baada kuwasili Ilala unatarajia kuzindua miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo miradi ya Afya , Barabara,vikundi vya kijamii na Lishe.


Ameongeza kuwa, mara baada kuwasili Ilala na kuzindua miradi ya Maendeleo Mwenge huo unatarajia kulala Jimbo la Ukonga eneo la Ukonga Mzambarauni Shule ya Msingi ambapo Burudani mbalimbali mziki wa kizazi kipya zitakuwepo.


Akizungumzia sehemu ambayo unalala Mwenge amesema pia kutakuwa na maonyesho ya bidhaa mbalimbali pamoja na upimaji Afya VVu UKIMWI na  Chanjo ya UVIKO 19.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI