Header Ads Widget

MBIO ZA KUITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA ZASHIKA KASI KUPITIA MISS UTALII TANZANIA, KWA UDHAMINI WA TFS




Ujio mpya wa shindano la Miss Utalii Tanzania, umefungua milango ya Tanzania kujitangaza kimataifa kupitia ushiriki wa washindi wa shindano hilo katika fainali za dunia za mashindano mbalimbali ya urembo wa kitalii na kitamaduni.



Ikumbukwe kuwa waandaaji wa shindano hili, wamefanya kazi kubwa ya kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia shinado hilo la Miss Utalii Tanzania kwa washindi wake wa kitaifa na wengineo wa ngazi mbalimbali kushiriki na kushinda mataji ya dunia katika fainali za dunia za mashindano mbalimbali, mafanikio ambayo yalipelekea Tanzania kupewa heshima ya kuwa wenyeji wa fainali za dunia za Miss Utalii Dunia 2006.




Baada ya kusitishwa kwa muda mwaka 2013/2014, na kuanza upya mwaka 2020/2021 baada ya kuboresha mfumo wa shindano na uongozi, tayali matunda yake yameanza kuonekana kwa kuanza kupeleka washindi wake wa mwaka 2021/2022 katika mashindano mbalimbali ya dunia ya urembo wa kitalii na kitamaduni. 



Ambapo mshindi wa pili wa Miss Utalii Tanzania 2021/2022, Judith Peter Ngusa , jana tarehe 02-5-2022 amesafiri kwenda nchini India kwa ndege ya shirika la ndege la Ethiopia Airline kushiri na kuwakilisha Tanzania katika fainali za dunia za Miss United Nation 2022,zitakazo fanyika tarehe 8-5-2022 jijini New Delhi India, kwa udhamini wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS).




Katika fainali hizo za dunia za Miss United Nation 2022, mrembo huyo wa Miss Utalii Tanzania 2021, ataungana na zaidi ya warembo 70 wakiwakilisha nchi zao katika kuwania taji hilo la Miss United Nation 2022, huku akitangaza vivutio vya utalii na uwekezaji wa kitalii vya Tanzania, lakini ajenda yake kuu ikiwa ni kutangaza vivutio vya utalii wa kiikolojia (TFS – Tanzania Eco Tourism tourist destinations) vya Tanzania kupitia ushiriki wake katika fainali hizo za dunia nchini India.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti mkurugezi wa Ufundi na Mashindano Georgina Saulo, kwa niaba ya manejimenti amewashukuru TFS, kwa kusaidia kufanikisha ushiriki wa warembo wa Miss Utalii Tanzania katika fainali hizo za Dunia, na kuahidi kuwa kufuatia udhamini huo sasa na kipekee Utalii wa Kiikolojia na vivutio vya Utalii vilivyo chini ya TFS ndio kipaumbele cha washiriki wa Miss Utalii Tanzania kimataifa na katika utekelezaji wa majukumu ya ushiriki na ushindi wao kitaifa na kimataifa.




Rais wa Miss Tourism Tanzania Beauty Pageant,Erasto Gideon kwa niaba ya bodi , amatoa shukurani na pongezi kwa uongozi na wafanyakazi wote wa TFS , kwa kutambua na kuthamini mchango wa Urembo wa kitalii na kitamaduni katika kukuza na kuendeleza sekta ya utalii na uhifadhi, hususani Utalii wa Kiikolojia, Maeneo ya Urithi wa Taifa na Kitamaduni.


 Aidha Ndugu amesisitiza kuwa, warembo wa Miss Utalii Tanzania mwaka huu  wamealikwa na kupewa heshima ya kushiriki katika zaidi ya mashindano kumi ya dunia na mengineyo ya kimataifa, katika nchi mbalimbali duniani barani Ulaya,Amerika,Asia na Afrika. 



Hii ni fursa kwa Tanzania na TFS kujitangaza kimataifa kwani kilashindano linashirikisha wastani wa nchi 100. Kitaifa tumeandaa program maalum ya promosheni ya utalii wa kiikolojia, mali kale, hifadhi za misitu za majini na nchi kavu itakayo julikana kama “Tanzania Eco Tourism and Conservation Great Safari Tour”.


All Correspondences should be addressed to President,Miss Tourism Tanzania Pageant,P.O.Box 72899 Dar es Salaam, Call/ What’sapp: +255 74816 7651Email:misstourismpresident@gmail.com, presidentmisstourismorganisation@yahoo.co.uk, missutaliitanzania@gmail.com




Hatua hii ni utekelezaji na uungaji mkono kwa vitendo juhudi za serikali na mamlaka zake za utalii na uhifadhi ikiwemo TFS katika kukuza na kuendeleza sekta ya utalii na uhifadhi, kama ilivyo idhihirishwa na kupambanuliwa katika filamu ya TANZANIA ROYAL TOUR iliyo fanywa na Mheshimiwa Samii Suluhu Hasani, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ILANI YA UCHAGUZI YA CHAMA TAWALA ya 2020/2025 na hotuba ya Waziri wa Maliasili na Utalii , Mheshimiwa Pindi Chana alipo tembelea makao makuu ya TAWA.


Kwa maandalizi tuliyo fanya tunaimani kubwa kuwa Judith Peter Ngusa sio atawakilisha vyema Tanzania tu, bali atadumisha na kuendeleza rekodi yetu Miss Utalii Tanzania ya kushinda mataji katika mashindano yote ya dunia na kimataifa tuliyo shiriki na kuwakilisha Tanzania.

 


Tunawaomba watanzania wote tumwombe ashinde Taji. Fainali ya Miss United Nations 2022, zinafanyika New Delh India tarehe 8-5-2022.Pamoja na taarifa hii,hapa naambatanisha picha za  mshiriki ,Judith Peter Ngusa, mshindi wa pili Miss Tourism Tanzania 2021 , mwakilishi wa Tanzania fainali za Dunia Miss United Nation 2022 Nina kuahakikishia ushirikiano bora daima.




Asante

Georgina Saulo

Mkurugenzi wa Ufundi na Mashindano – Miss Tourism Tanzania Beauty Pageants

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI