Katibu Tawala wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Saidi Kitunga amezindua awamu ya pili ya mbio za Transec Lake Victoria Marathon 2022 zitakazofanyika Juni 26 mwaka huu mkoani humo
Mratibu wa mbio hizo, Frank Sendwa amesema mbio hizo zitakazofanyika katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza zitajumuisha mbio ndefu ambapo washiriki watakimbia Kilometa 21 na Kilometa 2.5 kwa wazee, watu wenye ulemavu na wasiyojiweza.
Pia amesema washiriki wanatakiwa kulipa Sh35,000 kwa ajili ya vifaa vitakavyotumika katika mbio hizo.
Akizungumzia mbio hizo, Magreth Macha amesema zinalenga kusaidia utoaji wa Bima za Afya kwa watoto 100 walioshindwa kumudu gharama za matibabu ya maradhi hayo ili kuwawezesha kutibiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.
0 Comments