Header Ads Widget

DC WA MBINGA ATOA AGIZO KWA WAKURUGENZI

MKUU wa Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma Aziza Mangosongo amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri ya Mbinga mji na Mbinga Vijijini kwenda na kamati zao za Elimu  kujifunza mbinu za ujenzi wa Nyumba za Walimu wa shule ya Sekondari Kigonsera ili kufanikisha kutatua changamoto za upungufu wa Nyumba za Walimu.MWANDISHI AMON MTEGA MATUKIO DAIMA APP RUVUMA


Wito huo aliutoa jana kwenye mahafali ya 23 ya kidato cha sita katika ya Sekondari ya Kigonsera ambapo wahitimu 435 mkuu huyo alizindua  nyumba moja ambayo imegarimu zaidi ya sh.Milioni 74  na nyingine aliweka jiwe la msingi ambayo ujenzi wake unaendelea na upo hatua za mwisho.


Mangosongo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo alisema kuwa amefurahishwa na kazi inayofanywa na uongozi wa shule hiyo katika suala zima la uibuaji wa miradi mbalimbali yenye faida kwa shule hiyo ikiwemo ujenzi wa Nyumba hizo huku akiwataka Wakurugenzi wa Halmashauri hizo kwenda kujifunza.


Alisema kuwa mpango uliyofanywa na shule hiyo ya kuweka mikakati ya ujenzi wa Nyumba hizo ni mikakati ambayo inaleta tija kwenye shule hiyo hivyo kunakilasababu ya kuungwa mkono wakiwemo Wakurugenzi na wajumbe mbalimbali wakiwemo wa kamati za Elimu  kwenda kujifunza shuleni hapo .


Aidha mkuu huyo wa Wilaya baada ya kujionea jitihada zinazofanywa na shule hiyo aliwataka Wanafunzi wa shule hiyo kuacha tabia ya kuharibu  miundombinu mbalimbali ya shule hiyo na badala yake iweze kuangaliwa isiharibiwe.


Awali akitolea taarifa za ujenzi wa Nyumba hizo mkuu wa shule ya Sekondari Kigonsera Ponsiano Ngungulu alisema ujenzi huo umewashirikisha Wazazi na wadau wa Elimu pamoja na elimu ya kujitegemea inayofundishwa pia hapo shuleni ambao wote kwa pamoja wanachangia ujenzi huo.


Ngungulu alifafanua kuwa malengo ni kufikisha nyumba sita ambazo zinajengwa kwa mfumo wa moja kwa mbili na kuzifanya  familia 12 ziweze kuishi kwenye Nyumba hizo ambapo hadi sasa mpango huo unaenda vizuri kwa kuwa baadhi ya Nyumba hizo kukamilika na tayari zinakaliwa na watumishi wa shuleni hapo.

 


 Hata hivyo mkuu wa shule hiyo aliipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongonzwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea kuongeza nguvu katika sekta mbalimbali mbalimbali ikiwemo ya Elimu.

 

 Pia mkuu huyo licha ya kutoa pongezi hizo alibainisha baadhi ya changamoto zinazoikabili shule hiyo kama upungufu wa Walimu kwa baadhi ya masomo, upungufu wa Nyumba za Walimu licha ya mikakati ya ujenzi wa Nyumba hizo ukiendelea na upungufu wa vifaa vya kisayansi kwaajili ya kuwafundishia wanafunzi.

          



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI