Header Ads Widget

MATUKIO YA VITENDO VYA UKATILI KWA WANAWAKE NA WATOTO VYATAJWA KUPUNGUA KWA MWAKA 2020 HADI 2021.

 



Teddy Kilanga, Arusha.


Matukio vitendo vya Ukatili dhidi ya wanawake  na watoto nchini vimepungua kutoka 41673 hadi 29000  ikiwa kwa watoto ni 15870 hadi 11499 kwa mwaka 2020 hadi 202I.


Akizungumza wakati akitoa takwimu za matukio ya ukatili kwa waendesha mashtaka wa serikali na wadau wa sheria kutoka mikoa yote ya Tanzania,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha sheria haki za kibinadamu(LHRC)Fulgence Massawe amesema pamoja na hayo mwaka 2021 walipokea matukio ya mauaji ya wanawake yapatayo 30.


"Mauaji hayo ya wanawake hudaiwa kutokana na ukatili  wa majumbani wengine kudai ni wivu kimapenzi ikiwa taarifa hiyo imeonyesha kwamba ukatili wa kimwili kwa wanawake pamoja na watoto,"amesema Kaimu huyo.


Aidha ameongeza kuwa ukeketaji pia ni sehemu ya ukatili na mikoa ambayo imekuwa kinara ni pamoja Arusha,Mwanza ,Tanga na shinyanga  na Ilala ikiwa kituo cha LHRC kimekuwa kikifanya mifumo mbalimbali ya kuwajengea watu uwezo pamoja na kuhakikisha misingi ya utendaji kazi na uwezeshaji wa kisheria kwamba matukio hayo yanaisha kwa kuangazia nyanja mbalimbali.


"Kwa kuangalia nyanja hizo mbalimbali ikiwa kwa mwaka jana wamewajengea uwezo Maafisa wa ustawi wa jamii kwa mikoa yote ya Tanzania isipokuwa mkoa wa Manyara na Dar es Salaam ikiwa mwaka huu wameanza kuwajengea uwezo waendesha mashtaka ili wanapofanya kazi zao wafahamu namna ya kutatua,"amesema Massawe.


Amesema kuwa ,mwaka huu wameamua kuwajengea uwezo waendesha mashtaka wa serikali kutoka mikoa yote ya Tanzania lengo likiwa ni kuwawezesha kutoa haki kwa kufuata misingi ya sheria , kwa weledi na kuhakikisha kuwa wanasimamia vizuri masuala ya upatikanaji wa haki kwa Wanawake, watoto na walemavu nchini.


Kwa upande wake,Katibu Mkuu wa wizara ya katiba na sheria,Mary Makondo amesema  lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha wanajifunza namna bora ya kutatua changamoto ya ucheleweshaji na uendeshaji wa mashauri pamoja na kupunguza msongamano wa mahabusu magerezani.


" Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imeendelea kuboresha  uwezeshaji wa mafunzo kwa waendesha mashtaka  wa serikali ndani na nje ya nchi kwa lengo la  kusaidia  upatikanaji  wa  haki kwa wananchi  hususani katika masuala haya ya ukatili kwa wanawake, watoto na walemavu"amesema Makondo.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Sylvester Mwakitalu amesema kuwa, mwendesha Mashtaka ni kiungo muhimu katika kutoa haki nchini  na misingi yao ni kutenda haki.



Amewataka waendesha mashitaka hao baada ya mafunzo hayo serikali inatarajia kuona matokeo chanya (Impact) huku akiwataka kufanya Kazi kwa weledi, na uadilifu katika kuwasaidia wananchi kwenye suala zima la upatikanaji wa haki.


" Tumefanya utafiti baadhi ya mikoa lakini tumebaini matukio ya Ukatili ni mengi kuliko takwimu zinazozungumziwa, yapo matukio yanayofika polisi na kumalizika katika hatua hiyo bila kufika ngazi za waendesha mashtaka lakini pia yapo mengine yasiyoripotiwa kabisa lakini yanayofika katika ofisi ya waendesha Mashtaka ndiyo yanayotajwa katika takwimu ila  kiuhalisia matukio ni mengi " amesema.


Amewataka waendesha Mashtaka kuhakikisha ushahidi wa kutosha unakusanywa na kufanyiwa kazi vizuri kwa haki na kwa haraka ili kuwasaidia wananchi katika suala zima la sheria  ambapo  wadau wakubwa wa kuelimisha na kusaidia masuala haya wamekuwa  kituo cha  sheria na haki za binadamu kwa namna ambavyo wamekuwa wakitoa mafunzo ya sheria kwa wadau hao.


Kwa upande wa washiriki wa mafunzo hayo, Abdallah Chavula Mkuu wa Mashtaka mkoa wa Arusha amesema kuwa,  mafunzo hayo yatawasaidia  katika utendaji kazi wao kwani ni ya muhimu zaidi  katika kuendeleza taaluma yao.



Amesema  kuwa,uelewa wa wananchi bado ni mdogo katika sheria hata kusababisha matukio ya ukatili kumalizwa kimya kimya au kimila bila wadau wa sheria kuhusishwa,hivyo alitaka elimu zaidi kutolewa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI