Na Mwandishi wetu, Mtwara
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba, Kanda ya Kusini imeandaa bonanza kwa kushirikisha Taasisi zote zilizopo katika jengo la Sokoine PSSSF Mtwara ili kujenga mahusiano na kujiimalisha kiafya.
Bonanza hilo lililofanyika katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Ufundi maarufu kama Mwasandube ambapo Michezo iliyochezwa/kushindaniwa ni pamoja na Mpira wa Miguu, Wavu Aidha Michezo mingine ilishindanishwa ni Kuvuta kamba, kukimbia na yai kwenye kijiko.
Akizungumza kwenye bonanza hilo alikuwa Meneja wa TMDA Kanda ya Kusini Dkt. Engelbert Mbekenga alisema kuwa wameandaa bonanza hilo ili kuhamasisha michezo kwaajili ya Linda afya za wafanyakazi.
Alisema kuwa uwepo wa bonanza hilo utawezesha wafanyakazi kukutana na watu mbalimbali kutoka taasisi zingine ambazo zimeshiriki katika michezo hiyo.
Alizitaja taasisi hizo kuwa ni TBS, JATU, PSSF, TASAC, AMACHA, NMB, MOP SQUAD, MASU pamoja na SUMA JKT.
"Michezo ni afya tunaomba tuendelee kuhamasishana ili tuweze kushiriki kwa wingi na tuweze kufahamiana na kuzindua rasmi Umoja wetu pamoja na kujenga afya zetu" alisema Dkt Mbekenga
"Unajua mara nyingi tunakuwa kazini hatufanyi mazoezi fursa za Michezo kama hii ni ya kipekee tuitumie ipasavyo kwakujenga mahusiano pia"
0 Comments