Teddy Kilanga _Arusha
Waziri wa maendeleo ya jamii,jinsia wanawake na Makundi Maalumu Doroth Gwajima ameitaka jamii kuchukua hatua za kulipoti matukio ya vitendo vya ukatili katika jeshi la polisi kupitia dawati la jinsia ili kuweza kukomesha vitendo hivyo kwa kuchukua hatua za kisheria.
Akizungumza katika ziara yake ya uhamasishaji wa siku ya familia ambayo inaadhimishwa mei 5,2022 ambapo kauli mbiu yake ni Dumisha amani na Upendo kwa familia imara tujitokeze kuhesabiwa,Waziri Gwajima alisema lengo ni katika kukumbushana upendo na amani.
Gwajima alisema asilimia 100 ya kesi hizo zimekuwa zikitendewa haki kutokana na serikali kuwa makini katika hilo lengo ni kuondoa vitendo hivyo katika jamii ambavyo vimekuwa vikiwanyima haki watu wanaofanyiwa ukatili.
Aidha Gwajima alisema mkoa wa Arusha unajumla ya matukio 808 hivyo amelishukuru jeshi la Polisi kwa kubimarisha mifumo yao kwani yapo baadhi ya maeneo vitendo vya ukatili vipo lakini hawayaripoti matukio hayo kutokana na dhana ndogo ikiwemo kutokuwa na elimu ya kutosha.
"Wito wangu kwa jamii tunakwenda kuadhimisha siku ya familia mei 15,2022 na siku hii kila mkoa utaadhimisha kwa namna walivyopanga lengo kubwa ni sauti kufika kwa wananchi hivyo tunatarajia jeshi la polisi kupitia dawati la jinsia lipokee kesi nyingi sana,"alisema.
Alisema taarifa ya utafiti ya mwaka 2011 wa serikali ya Tanzania pamoja na shirika la Uncef inaeleza kuwa matukio ya ukatili yanatokea kwa watoto katika familia kwa asilimia 60 ambapo hubaki kuishi nayo bila kulipoti katika vyombo husika ikiwa asilimia 40 ni ule unaotokea nje ya familia.
"Na hapo mkumbuke karibu matukio elfu 11.5 yalilipotiwa kwa taarifa ya jeshi la polisi katika kipindi cha januari hadi Desemba 2021 ikiwa matukio ya ubakaji yalikuwa takribani 5800 ni vyema familia zikakaa na kujengeana tabia ya kuzungumza mustakabali wa familia katika maendeleo pamoja na kupinga ukatili unaotokea majumbani,"alisema.
Aliongeza kuwa jamii ikiungana vitendo vya ukatili vitamalizika kabisa na vitendo hivyo vikiendelea kumalizwa kifamilia watakuwa wanazalisha chuki yenye visasi katika jamii na ili kuondokana na hali hiyo ni vyema jamii ikafichua vitendo vya kikatili kwa lengo la kuchukua hatua.
Aidha alisema suala la matatizo yanayotokea mitaani ni jambo linaloungana na mfumo mzima wa malezi na makuzi.
0 Comments