Header Ads Widget

DKT CHUWA "MAANDALIZI YA SENSA YAMEFIKIA ASILIMIA 81"

 



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


MTAKWIMU Mkuu wa Serikali Dkt Albina Chuwa amesema kuwa hadi kufikia tarehe 9 Mei 2022 maandalizi ya Sensa yamefikia asilimia 81 huku maandalizi ya zoezi la kuwasajili makarani na wasimimizi wa Sensa yakiwa yamefikia asilimia 51.


Tarehe 5 Mai Mwaka huu serikali ilitangaza rasmi kuanza kupokea maombi ya kazi zamuda za makarani na wasimimizi wa Sensa ya Watu na makazi itakkayofanyika Agosti 2022  kwa Mfumo wa Kielektroniki


Akiongea na waandishi wa habari Jijini hapa wakati akitoa taarifa kuhusu mwenendo wa Maombi ya kazi za muda  za Sensa Katika Mfumo wa Maombi wa Kielektroniki Dkt Chuwa amesema Kati ya waombaji 119,468 yameshapokelewa na Ofisi ya Takwimu NBS ambapo waombaji 46,159 ni waajiriwa kutoka Katika sekta ya Umma na binafsi.


Dkt Chuwa amesema waombaji 14,393 wamejiajiri wenyewe na waombaji  58,916  ni wale ambao hawana ajira.


"Katika Maombi haya tumegundua baadhi ya changamoto ambazo waombaji wamekuwanazo Ni kutokujaza taarifa sahihi kama vile barua Pepe na namba za siku na hivyo kushindwa Kupokea neno la Siri na taarifa nyingine muhimu za kumuwezesha Mwombaji kuendelea kukamilisha Maombi yake," amesema Dkt Chuwa.

 

Pia ameeleza changamoto nyingine waombaji Kutokuwa na baadhi ya taarifa Kama vile nammba ya kitambulisho Cha Taifa Cha NIDA,Kutoambatanisha nyaraka za lazima kama vile cheti cha kuzaliwa na nyengine waombaji kuwa Katika maeneo yenye Mtandao hafifu hivyo kupelekea kupata tatizo la kutuma na kuhuisha Maombi.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI