Na Amon Mtega,Matukio Daima APP Ruvuma
MBUNGE wa Jimbo la Songea mjini Mkoani Ruvuma Dkt Damas Ndumbaro ambaye pia ni Waziri wa Sheria na Katiba amewatoa hofu wakazi wa Jimbo hilo wanaotumia kivuko cha kinachounganisha kata ya Matarawe na Mjimwema ambacho kimesombwa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali hapa Nchini.
Dkt Ndumbaro amewatoa hofu hiyo wakati alipokuwa ameenda kuangalia kivuko hicho ambacho kimekuwa kiungo muhimu kwa wakazi wa kata hizo mbili licha na baadhi ya wakazi wa kata nyingine hutumia kivuko hicho.
Akizungumza kwenye kufuatia kuharibika kwa kivuko hicho amesema kuwa jitihada zinafanyika za kuhakikisha kinafanyiwa ujenzi wa muda ili wakazi maeneo hayo waendelee kukitumia na baada ya siku chache kitafanyiwa ujenzi wa daraja ambalo litakuwa suluhisho la kukabiliana na maji mengi yanayotokana na mvua.
Waziri Dkt Ndumbaro ambaye aliongezana na Meya wa Manispaa ya Songea Michael Mbano amesema licha ya kuwaondoa hofu wakazi hao pia amempongeza mhandisi wa barabara za mijini na Vijijini (Tarura)Wilaya ya Songea Mkoani humo John Ambrose kwa jitihada za haraka katika kuhakikisha kivuko hicho kinafanyiwa matengenezo ya muda kwa haraka zaidi.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Songea Michael Mbano amesema kuwa haribifu mwingine unaotokea kwenye miundombinu mbalimbali ikiwemo ya kwenye madaraja na vivuko ni kutokana na baadhi ya Wananchi wanapofanya shughuli za kibinadamu wamekuwa wakitupia takataka kwenye mito jambo ambalo hupelekea miundombinu hiyo kuharibika.
Mbano kufuatia hali hiyo amewataka wakazi wa Manispaa hiyo kuilinda miundombinu hiyo isiendelee kuharibiwa ili iweze kudumu kwa muda mrefu jambo ambalo litasaidia kuokoa garama za mara kwa mara kutumia kwenye miundombinu hiyo.
Naye mhandisi wa barabara wa Wilaya ya Songea John Ambrose amemwambia Waziri na Mbunge huyo kuwa ili kupata suluhisho la kivuko hicho ni kujenga daraja ambalo litagharimu zaidi ya shilingi Milioni 300,nakuwa kwa sasa linafanyia matengezo ya muda wakati mpango wa ujenzi wa daraja ukiendelea.
0 Comments