Na Hadija Omari Matukio DaimaAPP Lindi
WAKAZI wa Manispaa ya Lindi Mkoani humo wameipongeza Serikali kwa kuchukua jitihada za haraka za kutoa chanjo ya matone ya polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ili kukabiliana na ugonjwa wa huo
Wananchi hao wameyasema hayo kwa nyakati yofauti walipokuwa wakizungumza na Matukio Daima kufuatia kuanza kwa kampeni hiyo ya chanjo ya polio Nchi Mzima inayotarajia kuanza leo April 28 hadi mei 1 mwaka 2022 kutaka kujua namna walivyoipokea.
kwa upande wake Bi. Sharifa Chawala alisema anaipongeza Serikali kwa hatua hiyo iliyochukua ya kutoa chanjo kwa watoto itakayoweza kuzuia kuingia kwa ugonjwa huo.
Nae somoe salumu alisema kuwa ili zoezi hilo liweze kuwafikia watoto wengi katika halmashauri hiyo ni muhimu kwa viongozi iongeze kufanya kampeni kwa wingi zaidi ili wazazi na walezi waweze kuelewa kwa undani umuhimu wa kinga hii kwa watoto wao.
Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi cha Halmashauri ya Manispaa ya Lindi chenye lengo la kujadili namna zoezi hilo litakavyoendeshwa kwenye manispaa hiyo mshauri wa chanjo ya polio-kutoka shirika la afya duniani, Bw.amani massay alisema kuwa kutokana na kampeni hiyo ya uchanjaji kufanyika Nyumba kwa nyumba na maeneo tofauti tofauti kwenye makazi ya watu kutatoa fulsa kwa watoto hasa wale waliozaliwa nyumbani na kushindwa kuhudhulia klinik kwa wakati kwa ajili ya kupata chanjo.
" kwa kuwa serikali haiwezi kutambua mtoto yupi amepatiwa chanjo na yupi hajapatiwa chanjo imeonelea utolewaji wa chanjo hii utafanyika kwa watoto wote waliopata kwa utaratibu wa chanjo wa kawaida na wale walio bado kupata ili kuwakinga na ugonjwa huo na hii ni kutokana na chanjo hiyo kutokuwa na madhara hata kwa mtoto alietoka kuchoma jana" alifafanua
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa manispaa hiyo Dkt. Stanford Mwakatenge alisema kuwa manispaa hiyo ya Lindi inatarajia kuchanja watoto wapatao Elfu 32,632
Hata hivyo alieleza kuwa hatua ya chanjo hiyo kufanyika nyumba kwa nyumba itawaza kuongeza idadi ya utoaji wa chanjo hiyo ambayo kwa sasa katika utoaji wa kawaida imefikia asilimia 90% ya watoto wote waliozaliwa
Awali akifungua kikao kazi hiko Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shahibu Ndemanga alisema kuwa utolewaji wa chanjo hiyo ni kutokana na uwepo wa Mlipuko wa ugonjwa wa polio Nchi jirani ya Malawi ambapo baada ya Serikali kuona changamoto hiyo ikaamua kutoa chanjo ya polio kwa watoto ambao ndio waathirika wakubwa.
"Tumeamua tufanye kampeni ya kutoa chanjo ya ugonjwa huu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ambao wameonekana kama ndio wanaathirika zaidi , hivyo niwaombe tukitoka hapa kila mmoja aone kwamba kuna wajibu wa kwenda kueleza jambo hili kwa wananchi ili wajitokeze kwa wingi kuwatoa watoto wao waweze kupata chanjo hiyo" alisema Ndemanga
Mwisho
0 Comments