Header Ads Widget

UZALISHAJI WA KOROSHO MSIMU WA 2020/21 UMESHUKA TANECU


Na Matukio Daima APP Mtwara

Meneja Mkuu wa chama Kikuu cha Ushirika cha Tandahimba & Newala Cooperative Union (TANECU)  Mohamed Nassoro amesema kuwa

uzalishaji wa korosho umeshuka kwa asilimia 13 kutoka tani 59,049 mwaka 2019/2020 hadi tani 51,444 mwaka 2020/2021.

Ambapo mauzo hayo yalifanyika  katika minada 15 ya wazi ambapo mnada wa kwanza ulifanyika tarehe 09.10.2020 na wa mwisho tarehe 15.01.2021, katika msimu wa 2020/2021 zaidi ya kilo 51,444,010 zimezalishwa na kuuzwa kwa thamani ya Shilingi 119,515,098,991.


akizungumza katika  Mkutano Mkuu wa 27  wa chama  hicho alisema kuwa katika  minada hiyo iliwashirikisha wakulima ,viongozi mbalimbali, Bodi ya Korosho Tanzania, Soko la Bidhaa Tanzania na wadau mbalimbali wa tasnia ya korosho.


Alisema kuwa katika kiasi hicho cha korosho kilichozalishwa na kuuzwa , korosho za daraja la kwanza zilikuwa tani 48,589 na daraja la Pili tani 2,854.


Katika msimu huu uzalishaji kiwilaya ulikuwa Tandahimba tani 29,451 kutoka tani 37,628 msimu 2019/2020, ambayo imeshuka kwa asilimia 22 (22%) ikilinganishwa na msimu uliopita katika wilaya  Newala tani 21,992 kutoka tani 21,421 msimu 2019/2020.


Kwa sasa imepanda kwa asilimia 2.3 (2.3%) ikilinganishwa na msimu uliopita. 


Aidha, Kutokana na kushuka kwa uzalishaji wa korosho TANECU LTD imepanga 


kuajiri Maafisa Ugani ambao watakuwa wakishirikiana na Maafisa kilimo Wilaya za 


Newala na Tandahimba katika kuwashauri wakulima juu ya mambo mbali mbali yanahusu kilimo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI