Na Teddy Kilanga MATUKIO DAIMA APP ARUSHA
Katibu Mkuu Taifa wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM)Kenani Kihongosi amezitaka wazara zilizopewa dhamana ya kusimamia maslahi ya vijana kujitathmini katika kutimiza wajibu wao kwa vijana nchini.
Akizungumza katika kongamano la umoja wa vijana wa mkoa wa Arusha,Kihongozi amesema ni vyema wizara zenye dhamana zikatekeleza wajibu wao kwani kwa sasa hawaoni wanachofanya ikiwemo pamoja na kuandaa makongamano yanayowahusu vijana.
"Tunawatizama kwa jicho kali kwelikweli na tusipozungumza wataendelea kukaa ofisini na kuzunguka na magari ya serikali hivyo tunawataka watoke wakazunguke kwa vijana ili kufahamu changamoto zinazowakumba vijana,"amesema Kihongosi.
Amesema wakae wakifahamu umoja wa vijana hawaogopi na hawataweza kuogopa ikiwa yoyote anayemkanyaga kijana watamkanyaga bila kuangalia mbele wala nyuma kwani huwa wanaambiwa kuna mifuko inayotoa fedha kwa vijana hivyo ni vyema wakawaeleza namna zinavyopatikana ili vijana waweze kujiajiri.
"Kila siku mtasomewa taarifa za fedha zinazohusu vijana lakini ukiwauliza vijana wanakana na kumekuwa na baadhi ya mchwa wanaokula hizi fedha ikiwa sasa tumeshakubaliana kuunda taxforce ya kufanya ukaguzi wa fedha za vijana nchi nzima kupitia halmashauri zote 195,"amesema Kihongosi.
Aidha amesema lengo la kamati hiyo ya ukaguzi wa fedha za vijana ni kwa lengo la kufahamu zilivyotumika na kuwafikia walengwa kwasababu wanauhakika ya baadhi ya fedha kutofika kwa walengwa ikiwa jambo hilo watakwenda kulisimamia ili kuhakikisha wizara hizo zinatekeleza wajibu wao kwa vijana.
0 Comments