Header Ads Widget

ASKOFU GAVILE ;TULIOMBEE TAIFA NA VIONGOZI WAKE ILI WAONGOZE KWA KUTANGULIZA HOFU YA MUNGU

  


Askofu wa Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa Blaston Gavile akitoa Baraka za Pasaka Kwa waumini wa Kanisa hilo Usharika wa Kanisa kuu wakati wa ibada ya pili ya jumapili ya Pasaka kanisani hapo 

 NA MATUKIO DAIMA APP,IRINGA
ASKOFU  wa  kanisa la   kiinjili la  kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya  Iringa Blaston Gavile  ametaka   watanzania   kuendelea  kuliombea  Taifa  ili   kuepuka  machafuko ya kivita kama  yanayoendelea  kati ya   Taifa  la  Ukrein na Urusi  kwa  kuwa  madhara  ya  vita   hiyo ni makubwa  kwa binadamu  kupoteza maisha na mali  kuendelea kuharibiwa  pia  kuombea  viongozi  ili wawe na  hofu ya  Mungu katika  kuongeza Taifa .

Askofu   Gavile   aliyasema hayo  Leo  wakati  akitoa  salamu  za Pasaka kwa  kanisa  hilo  kupitia waumini  wa  usharika  wa kanisa  kuu ,  alisema kuwa  wakati   waumini  wa kanisa  hilo  dayosisi ya  Iringa   wauaungana na   kikristo   kote  ulimwenguni   katika  kusherekea   sikukuu ya  Pasaka   kuna  kila sababu kwa  watanzania  kumshukuru  Mungu  kwani  nchi ina  amani na utulivu  wa  kutosha  .

" Wote  tunafahamu  kinachoendelea katika  nchi  nyingine  mathalani  vita ya  Urusi  dhidi ya  Ukraine   watu  wanapoteza maisha  na  waathirika   wakubwa  ni  watoto ,wazee  na  wanawake  lakini  tunaona namna ambavyo miundo mbinu  inavyoharibika kutokana na  silaha  nzito ambazo majeshi  yanatumia" 

 Alisema  kwa  mujibu  wa  takwimu  za umoja  wa  mataifa (UN)  watu  zaidi ya  20,000 wamepoteza maisha na maelfu   ya watu wanakimbia  nchini humo  kwa  kukosa amani  na  utulivu pia  gharama  za  maisha ikiwemo  ya  nishati ya mafuta ya  imepanda   duniani  kote  ambapo tunashuhudia  bidhaa kama  unga wa ngano ,mafuta ,huduma  za  usafirishaji  zikipanda  na  kusababisha  usumbufu  kwa  wananchi .


Askofu  Gavile  alisema  jambo la  msingi  kwa  waumini  wa kanisa  hilo  ni kuomba Mungu aimalishe  am,ani na utulivu ili  watanzania wasiwe  watu  wa  kulalamika  au  kushabikia mambo  badala yake kuwa  watu  wa kufunga na kuombea amani na  utulivu  nchini   izidi  kuendelea kudumu  kama  ambavyo viongozi  waasisi  wakuu wa Taifa   la Tanzania kama hayati baba wa Taifa Julius Nyerere  Abeid Aman Karume  walivyoweza  kuacha amani na utulivu.

"  Tuwaombee  viongozi  wetu kuanzia  Rais Samia  Suluhu  Hassan  ,makamu  wa  Rais Dkt  Philip  Mpango, waziri  mkuu Kasim  Majaliwa ,spika  wa  bunge  Dkt  Tulia Ackson na  viongozi  wengine  ili  Mungu  awape  afya  njema  ,hekima,busara  katika  kuongoza Taifa  letu ili lifuate misingi  ya  utawala bora  na  kuleta maendeleo  kwa Taifa"


HALI  YA  UKATILI KATIKA  JAMII
Alisema  kuwa  kanisa ,jamii ,mashirika na  wadau  wengine  kwa  pamoja  hakuna  budi kushirikiana  na  serikali  kutokomeza  vitendo vya ukatili  katika  jamii .

Askofu  Gavile  alisema  ripoti  ya  jeshi la  polisi  ya  mwaka 2020 inabainisha  ukatili  wa  ubakaji   kwa  watoto   kwa  kuwa na  visa  7,263 vilivyoripotiwa  ikiwa  ni  ongezeko la asilimia 26 ikilinganishwa  na  mwaka 2015  mwaka ambao  viliripotiwa  visa  5803   kwa   hii  ni  ikiwa ni sawa na  visa  615  kwa  mwezi jambo  ambalo  linahatarisha mustakabali  wa  ustawi  wa  watoto  .

"Kwa siku  za  karibuni   kumekuwa na ongezeko   la matukio ya ukatili  katika  jamii  yakiwemo ya  ubakaji ,ulawiti wa  watoto  ,vipigo kwa wanawake na  mauwaji  ya  kikatili  kuwa  Roho   hii ya ukatili  imeongezeka kutokana na  watu   kukosa   upende na  hofu ya  Mungu  kwa   kutoheshimu na  kuthamini  uumbaji  wa Mungu  pia tamaa ya  mali  na imani  za  kishirikina ni  miungoni  mwa  mambo  yanayochangia  kuongezeka kwa  ukatili  huu katika  jamii"

Hata  hivyo  alipongeza  idara ya familia na malezi  KKKT Dayosisi ya  Iringa  kwa kuendelea  kuzunguka katika  sharika  zote  kufanya  semina kwa watoto ,wazazi na  walezi  juu ya  ukatili  ,mafunzo ambayo  yataamusha ari  na  uelewa wa  kupinga  vitendo vya  ukatili  ambavyo vinaendelea kinyume na mpango wa  Mungu.

Pia  aliomba  waumini  wote  wa kanisa  hilo  wanaposherekea Pasaka  kuingia  katika toba ya kweli juu ya umwagaji damu  zisizo  na hatia nchini  Ukrein  kwani  ni chukizo  kwa  Mungu  pia kuomba  kwa ajili ya vitendo vya  ukatili  vinavyoendelea  nchini na  kuombea Taifa amani .

MABADILIKO  TABIA  NCHI.

Alisema  kuwa  mabadiliko  Taibanchi  ni  miongoni mwa  changamoto  kubwa   inayoikumba dunia  kwa sasa  ambayo  inasababisha  kupungua kwa misitu ,mabadiliko ya utaratibu wa mvua na  kuongezeka kwa  kiwango  cha maji ya bahari  kunaweza kuongeza  shinikizo la  kiuchumi ,kisiasa  na  kijamii  lililopo  na   kuathiri  maendeleo ya  jamii .

Kuwa  mwaka  huu   Taifa  limeshuhudia mvua  ikichelewa  kuanza  kunyesha na maeneo mengi  hali  inaonesha mazao  mengi huenda  yasikomae  kwa  kiwango  sitahiki  hali  ambayo   inaashiria huenda  kukawa na upungufu  wa  chakula  hivyo  wakuu wa majimbo ,wachungaji  na  viongozi  wengine  wa kanisa na jamii   wanapaswa  kuelimisha  wananchi  kutunza  chakula  watakachovuna pia  waliopo mabondeni   ambako  kuna ruhusiwa kulima  basi  wasisite  kupanda  mazao  ya muda mufupi  kwa   ajili ya kukabiliana na hali   hii ya  hofu ya  chakula.



SENSA YA  WATU NA MAKAZI

Askofu  Gavile  alisema kuwa  serikali  ya jamuhuri ya  muungano wa Tanzania  imepanga  kufanya  sensa  ya  watu na makazi  ifikapo mwezi Agosti  mwaka huu 2022 kuwa  sensa   ya mwaka 2022 itakuwa ni  sensa  ya sita kufanyika  nchini  baada ya muungano  wa Tanganyika na  Zanzibar  mwaka 1964   wakati  sensa  nyingine  zilifanyika  mwaka 1967,1978,1988 ,2002 na  2012.

"  Zoezi  hili  liliasisiwa  tangu enzi   na  enzi   Tukisoma katika  Biblia  takatifu  katika  vitabu  vya  hesabu na  Injili  zote  nne (  Luka ,Marko ,Mathayo  na  nyingine   kuhesabu  watu  ni jambo la  kawaida  katika jamii  yoyote  ile   yenye malengo chanya  hata wana  wa Israel  pamoja na  wazazi wa Yesu Kristo  walihesabiwa  hivyo kanisa  tuendelee kuelimisha  washarika  wetu  kushiriki  zoezi la kuhesabiwa  kwa  ukamilifu  muda  utakapofika na  kujiepusha na  dhana ya upotoshaji  kwani  Sensa ni muhimu  sana"  alisema askofu Gavile .

Alisema  sensa  huisaidia serikali  kupata taarifa  za msingi  zitakazosaidia mchakato wa  utekelezaji wa  dira  ya maendeleo  ya mwaka 2025 ,mageuzi ya ,masuala ya afya na jamii ,pamoja na  ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo  za  kimataifa kwani  taarifa  za  idadi ya  watu  husaidia katika  mamalaka za  wilaya  katika  utekelezaji wa mipango ya  maendeleo ambayo huakisi matakwa  ya  watu  katika  ngazi  husika  na kusaidia kwenye uwiano  wa  mgawanyo  wa raslimali  hivyo  kila  mmoja  aendelee  kuombea  zoezi la sensa kufanyika kwa ufanisi  zaidi .
















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI