Header Ads Widget

RPC LINDI, ATAADHARISHA WATOTO KWENDA KWENYE FUKWE ZA BAHARI BILA UANGALIZI WA WAZAZI

 

 NA HADIJA OMARY,MATUKIO DAIMA APP LINDI 

KAMANDA  wa Polisi Mkoa wa Lindi, ACP Mtatiro Kitinkwi amewataka Wazazi Mkoani humo hasa wanaoishi kwenye mwambao wa bahari ya Indi kutoruhusu watoto wadogo kwenda peke yao Baharini bila uangalizi wa mtu mzima


Kitinkwi ametoa wito huo mara baada ya kukagua gari za Abiria katika kiziwizi cha Magari Mjini hapo,  Bara bara kuu ya magari  kutoka Mtwara kwenda Dar na kuzungumza na baadhi ya Abiria 



Kitinkwi alisema kuwa baada ya Serikali kupiga marufuku ya kuwepo kwa Disco toto wakazi wa Mkoa huo ikiwemo watoto utumia fukwe za bahari kucheza michezo mbali mbali


Alisema ni marufuku kwa wazazi kuwaacha watoto wanaenda kwenye fukwe za Bahari wakiwa hawana uangalizi wa watu wakubwa kwani kitendo hiko kina hatarisha maisha ya watoto hao hivyo ni wajibu wa Mzazi kuchukua taadhari kabla ya Mtoto wake kuondoka


Hata hivyo pamoja na mambo mengine kamanda Kitinkwi aliwataka Madereva wa vyombo vya Moto kutotumia vileo wanapoendesha vyombo vya moto sambamba na kuzingatia sheria za usalama barabarani  huku akiwataka watumia bara bara kuwa waangalifu wa wapo barabara 


Kwa upande wake Rashidi pukwa Dereva wa gari ya buti la Zungu alilipongeza jeshi hilo kwa kuendelea kutoa Elimu ya usalama barabarani kwani kama madereva uwasaidia kuwakumbusha mambo mbali mbali ya usalama wa Barabarani 


Nae Mariamu juma alisema kuwa swala la uangalizi wa watoto kwa Wazazi ni muhimu sana sio tu kwenda nae bari hata kufuatilia michezo wanayoicheza hapo


" wapo baadhi ya wazazi wanawaacha watoto wakiongozana na watoto wenzao mfano mtoto wa miaka 10 au tisa ukimkabidhi mtoto mwenzie wa miaka mitatu minne wakifika kule wote akili zao zinahamia kwenye michezo ndo matokeo yake Mtoto anapotea au hata wakati mwingine anaweza kuzamia hata baharini kwahuyo uangalizi wa wazazi kwa watoto ni muhimu sana sana"

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI