Na Matukio Daima APP
KAMISHNA msaidizi wa Ardhi mkoa wa Dar Es Salaam Idrisa Kayera amewataka wananchi kushiriki katika zoezi la upimaji linaloendelea katika wilaya mbalimbali katika mkoa huo na amesisitiza uwepo wa nyaraka muhimu wakati wa zoezi hilo hasa mikataba ya mauziano ardhi baina yao ili kurahisisha upimaji kufanyika kwa haraka na uhakika
Kayera amesema wakazi wa Dar Es Salaam wengi wanaishi katika maeneo ambayo hayapimwa na kupangwa katika utaratibu wa mipango miji, amesema zoezi hili limeanza kwa mafanikio makubwa sana kwani mpaka sasa mitaa mingi imeshatambuliwa na kupangwa hususani kwa wananchi waliotimiza vigezo vya upimaji
Mpaka sasa mitaa 270 ambako urasimishaji unafanyika na tayari mitaa hiyo imeshatambuliwa katika Wilaya zifuatazo ambapo Ilala ina mitaa 110, Kigamboni ina mitaa 19, Kinondoni ina mitaa 33, Temeke ina mitaa 44, Ubungo ina mitaa 64 amesema katika taratibu za mipango miji zoezi limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani zaidi ya vipande 604571 na tayari michoro 1998 imeshaandaliwa na viwanja vilivyoainishwa ni 523353
Amesema wananchi wanapojitokeza kushiriki ni faida kwa pande zote mbili ambapo amesema wananchi wanaweza kutumia Hati zao katika masuala mbalimbali nje ya utatuzi wa migogoro ikiwa ni pamoja na dhamana kwenye Taasisi za fedha pindi wanapohitaji mikopo
Kamishna huyo mesema gharama za upimaji zimepungua sana, haizidi asilimia 0.5 ambapo mwananchi yeyote anaweza kumudu gharama hizo
Jumla ya maombi 16000 yaliwasilishwa ofisi ya kamishna na tayari zaidi ya Hati 14000 zimekamilika na Hati 9818 zimeshachukuliwa na wananchi wa mkoa wa Dar Es Salaam
Kayera amesema haya yote ni mafanikio ya Raisi wa awamu ya sita katika kuhakikisha wananchi wa mkoa wa Dar Es Salaam wanamiliki Hati kwa usalama wa miliki kwa wananchi na kuepuka usumbufu kama ilivyokuwa awali
Aidha mratibu wa urasimishaji mkoa wa Dar Es Salaam Laurent Mswami amesema wananchi wanatakiwa kuzitumia vizuri ofisi za manispaa zote kwa ajili ya kupata elimu ya umiliki ikiwa ni pamoja na faida zake kwani kutokapimiwa kuna madhara mengi ambayo yanaweza kujitokeza huko mbeleni
Mswami amesema asilimia kubwa ya wananchi hukosa fedha kwa ajili ya kulipia upimaji na kusababisha kuzorota kwa zoezi katika maeneo mbalimbali, amawataka wananchi kutumia fursa ya kupimiwa kwa muda mfupi sana tofauti na awali, kwani endapo kila kitu kikiwa tayari kwa maana ya nyaraka mtu hujipatia Hati ndani ya siku moja na endapo itazidi sana haizidi wiki moja
"Natoa rai kwa wananchi kushiriki zoezi la upimaji kwa faida yao, endapo utapima na kupata Hati zipo faida nyingi ambazo wananchi watazipata ikiwa ni pamoja na kuongeza vipato kupitia Taasisi za fedha" alisema na pia amewataka wananchi wote wa mkoa wa Dar Es Salaam wanaoishi kwenye maeneo yasiyo rasmi kuhakikisha wanaingia katika zoezi la urasimishaji ili kupata hati itakayowawezesha kiuchumi na kusisitiza kuwa suala hilo linafanyika kwa nia njema kwa nia ya kuwaongezea mtaji wananchi kwa kupatiwa nyaraka itakayowasiadia kukopa fedha benki
0 Comments