NA MATUKIO DAIMA APP, DAR.
SAKATA la Wafanyakazi wa mtandao wa Habari za Umbea wa Mange Kimambi App uliorusha maudhui yasiyofaa wamefikishwa Mahakamani katika Mahakama ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam,
Aliyefikishwa Mahakamani ni Mkurugenzi wa Uturn Collection, Allen Salum Mhina (31), anayeishi Temeke ambapo mtandao huo wa Uturn collection na Mange Kimambi App, zimeshtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa makosa matatu likiwemo la kuchapisha maudhui hayo ya kuingilia uhuru wa mtu mwingine.
Mashtaka mengine waliyosomewa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate ni kufanya kazi ya uandishi wa habari bila kuwa na kibali na kutoka bodi ya ithibati ya wanahabari na kumfedhesha mtu kwa njia ya mtandao (cyber Bullying)
Hata hivyo upelelezi katika kesi hiyo namba 57 ya mwaka 2022 umeishakamilika na mshtakiwa Mhina anatarajiwa kusomewa maelezo ya awali (Preliminary Hearing) Aprili 27, 2022.
Mawakili wa Serikali waandamizi Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Sylivia Mitanto imedai Machi 9, 2022 katika maeneo tofauti ndani ya nje ya nchi ya Tanzania washtakiwa walichapisha video ya aliyekuwa Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay akiwa [ICU]. Mshtakiwa yuko nje kwa dhamana
Hata hivyo kupitia mtandao wa Kijamii wa Instagram kwa mangekimambi_ ameweza kuandika walaka wenye mabandiko mawili akilalamikia hali iliyotumika ikiwemo tukio la kufikishwa Mahakamani ndugu yake huyo.
0 Comments