Teddy Kilanga, Arusha.
Serikali imezindua mpango wa malipo ya tiketi kwa mtandao utakoanza kwa majaribio kesho April 1 , 2022 nchi nzima kwa lengo la kuboresha huduma za usafirishaji .
Akizungumza Jijini Arusha na Mkurugenzi wa huduma za uchukuzi wizara ya ujenzi na uchukuzi,Aron Kisaka wakati akiongea na wadau wa usafirishaji katika mikoa ya Manyara na Arusha.
Amesema kuwa, lengo la mkutano huo ni kutoa elimu kuhusiana na elimu ya tiketi mtandao ili wamiliki wote wa mabasi waweze kujua maana ya tiketi mtandao na hatua wanazoweza kuzichukua kuhakikisha wanajiunga na mfumo huo.
Ameongeza kuwa, wataendelea na majaribio hadi June 30 na katika kipindi hicho angalia changamoto na kuzitafutia ufumbuzi ili zikianza kutumika rasmi julai 1 rasmi wamiliki na wadau wote wanaotarajiwa kukata tiketi wawe na elimu hiyo.
"Baada ya kipindi hiki cha majaribio hakuna mtu yoyote anatakayetozwa faini ili hakikisha wote kuwa katika ukurasa mmoja,baada ya kipindi cha majaribio watakuwa Sasa mtu anayefanya makosa anatozwa faini."amesema .
Ameongeza kuwa,wasafiri wengi wanakutana na changamoto wakati wa kusafiri kutana na wapiga debe na kuwauzia tiketi kwa bei ya juu na wakati mwingine wanawauzia gari ambalo haliendi Safari hiyo ,ila uwepo wa mfumo huo watalipia tiketi yake kupitia simu ya mkononi halazimiki kwenda kituoni atafanya malipo kupitia simu na wale ambao hawana simu janja watatumia mawakala wa simu na kukata tiketi hizo na kuepuka adha ya wapiga debe.
Naye Mkurugenzi udhibiti usafiri kutoka mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA)Johansen Kahatano amesema kuwa, hapo awali walikutana na wadau mbalimbali wakiwemo Taboa, na TRA kuhakikisha changamoto zote zilizokuwa mwanzoni zimeisha ila wameona kabla ya kuanza waanze na wasafirishaji hao lengo likiwa kutoa elimu kuhusu tiketi mtandaoni ili liweze kutumika kwa umakini zaidi.
Kahatano amesema kuwa , wataendelea kutoa elimu hiyo mkoa wa Dodoma,Mwanza kazi kubwa ikiwa ni kutoa elimu katika kwenda kwenye utaratibu huo mpya huku lengo likiwa ni kuwa na mfumo unaofanana.
"Kazi ni kutoa elimu kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali kama TRA hivyo wameendelea kutoa elimu kwa wasafiridhaji itasaidia zoezi hili kuendeshwa kwa wepesi zaidi,"amesema.
Kwa upande wake, Meneja wa LATRA mkoa wa Arusha,Amani Mwakalebela amesema kuwa, Latra mkoa wa Arusha inatarajia kutoa elimu kwa wadau wa usafirishaji na wasafiri ili waelewe mfumo mpya wa ulipaji tiketi kwa njia ya mtandao na njia ya mabenki pindi wanapotaka kusafiri.
Amesema kuwa, LATRA pia itaendelea kutoa elimu kwa njia ya vyombo vya habari na mikusanyiko ili wananchi waelewe umuhimu wa kutumia tiketi mtandao ili kuepuka usumbufu wa wapiga debe ambao wamekuwa wakiwaibia kwa kuongeza gharama za usafiri na wakati mwingine kuwakatia siti moja watu wawili ,hivyo wataepukana na usumbufu huo na pia kuwa na uhakika wa fedha halali watakayolipia.
Kwa upande wa Katibu mtendaji kutoka Chama Cha wasafirishaji mkoa wa Arusha na Kilimanjaro(AKIBOA),Saidi Sharifu amesema kuwa hawakubaliani na mfumo huo kwani wanaona wanataka kutozwa kodi mara mbili katika biashara moja ,hivyo wameomba serikali ifanye maboresho zaidi ikiwemo kuwashirikisha wadau ili waelewe kwa mapana zaidi.
0 Comments