Header Ads Widget

TANECU YAPONGEZWA KWA KUANZISHA KIWANDA CHA UBANGUAJI KOROSHO

 



Na Mwandishi wetu, MATUKIODAIMA APP _Tandahimba


Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanal Patric Sawala  amekipongeza chama Kikuu cha Tandahimba & Newala Coperative Union (TANECU) kwakuona umuhimu wa kubangua korosho kwa kuanzisha kiwanda cha ubanguaji ambacho kitaleta mapinduzi katika tasnia ya korosho nchini.


Kauli hiyo ameitoa jana kwenye mkutano mkuu wa 27  wa chama hicho uliofanyika wilayani tandahimba ambapo alisema kuwa ubanguaji huo utakuza uchumi wa  wakulima na nchi kwa ujumla kwa kuacha kuuza korhso ghafi nje ya nchi.


“Niwapongeze tanecu kwa kuona umuhimu wa kuacha kuuza korhso ghafi na kujikita katika ubanguaji wa korosho na kuanzisha ujenzi wa kiwanda cha kubangua korosho hii itasaidia wakulima na kuongeza ubanguaji wa korhso nchini “


“Simamieni ubora wa korhso ili kutoruhusu korohso mbovu kuuzwa kutoka katika maghala yetu kama msimu uliopita ambao tuliuza korhso nzuri bora zenye viwango vinavyotakiwa


“Wapo wajanja wajanda kwenye pembejeo hata msimu uliopoita mlijitahidi kusimamia na kuwachukua hatua wanaofanya ujanja kwenye pambejeo naamini kwa msimu huu hazitakuja pembejeo za bure lakini naamini kuwa upo utaratibu madhubuti utakaotumika ili kuhakiisha kuwa kila mkulima anapata kwa maelekezo ya takayotolewa na seikali”


“Tuhamamsisha watanzania kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili kukuza uchumi wetu ambapo tutaongeza thamani ya mazao yetu na kuongeza ajira kwa watanzania walio wengi


Kwa upande wake Meneja Mkuu wa TANECE LTD Mohamed Nassoro alisema kuwa katika msimu wa 2020/21 wilaya ya Tandahimba ilizalisha  tani 29,451 kutoka tani 37,628 msimu 2019/2020 ambayo imeshuka kwa asilimia 22 (22%) ikilinganishwa na msimu uliopita huku  wilaya ya Newala tani 21,992 kutoka tani 21,421 msimu 2019/2020, ambayo imepanda kwa asilimia 2.3 (2.3%) ikilinganishwa na msimu uliopita. 


 


“Kutokana na kushuka kwa uzalishaji wa korosho TANECU LTD imepanga 


kuajiri Maafisa Ugani ambao watakuwa wakishirikiana na Maafisa kilimo Wilaya za 


Newala na Tandahimba katika kuwashauri wakulima juu ya mambo mbali mbali 


yanahusu kilimo. Pia, tutaanzisha vitalu vya kuzalisha miche ya mikorosho kwa ajili ya 


kuigawa kwa wakulima wa Newala na Tandahimba”


 


“Katika Msimu wa 2020/2021 mauzo ya korosho yalifanyika kwa kutumia mifumo 


miwili ambayo ni SANDUKU (TENDER BOX) chini ya uratibu wa Vyama Vikuu vya 


Ushirika na NJIA YA MTANDAO (ONLINE TRADING SYSTEM) chini ya uratibu 


wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX). Kupitia Mifumo hiyo miwili korosho zote ziliuzwa 


kama nilivyoeleza hapo juu. Aidha, kiasi cha tani 46,541 sawa na asilimia 91 kiliuzwa 


kwa njia ya SANDUKU na tani 4,902 sawa na asilimia 9 kiliuzwa na Soko la Bidhaa 


Tanzania (TMX”


Mkurugenzi wa Bodi  ya koorosho Tanzania  Francis Alfred alisema kuwa kwasasa bodi imejipanga kuzungumza na wanunuzi ili wakulima waweze kupata bei nzuri katika msimu huu.


Tunaangalia kwa sasa mnunuzi akija atoe bei nzuri ndio maana sisi tunasimamia ubora wa korhso zinazokuja sokoni hata ukianglaia bei zetu ziko juu ya wastani ukilinganisha na nchi zingine ndio maana tunahamasisha ubanguaji ambao utawezesha nchi kupata mapato”


“mimi nipongeze huu mpango wa TANECU kuanzisha kiwanda utasaidia kwa kiasi kikubwa nchi yetu kuuza korosho kwa bei nzuri na kuwezesha wakulima kupata pesa nzuri zaidi ya kuuza korosho ghafi” alisema Alfred


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI