.
Na,Jusline Marco Matukio Daima APP Arusha
Afisa Elimu jiji la Arusha wa elimu ya Ufundi Anthony Mushi amesema serikali bado ina kazi kubwa ya kuhakikisha inashirikiana na taasisi binafsi za elimu katika kutoa fursa kwa vijana kujifunza masomo ya sayansi ikiwa ni sambamba na walimu kufundishwa masuala ya sayansi ili nao waweze kuwafundisha wanafunzi kwa kiwango kikubwa.
Mushi ameyasema hayo katika maonesho ya Sayansi,Teknolojia na Mahesabu yaliyofanyika jijini Arusha,ambayo yameandaliwa na Taasisi ya E3 empower Aftika na kufadhiliwa na KOICA, amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wanajifunza masomo ya sayansi wangali wadogo ili yaweze kuwasaidia pindi watakapokuwa wakubwa hasa katika kujiajiri wenyewe kwani watakuwa na uelewa wa masuala ya kisayansi.
"Tunazungumzia masuala ya changamoto za ajira lakini vijana wetu wakiweza kusoma ICT kuna baadhi ya mambo wanaweza wakayafanya na wakaweza kuendesha maisha yao bila kutegemea serikali au mtu binafsi kuwaajiri."Alisisitiza Afisa huyo wa elimu Ufundi
Vilevile amesema pamoja na taasisi hiyo kutoa ushirikiano kwa serikali bado shule nyingi za serikali zinazofanya mitihani ya ICT ni chache ambazo hazizidi shule 5 katika jiji la Arusha kutokana na upungufu wa vitendea kazi na utayari wa wanafunzi na walimu kwa ajili ya kujifunza
Kwa upande wake George Mushi Mhandisi Mwezeshaji wa Mradi katika Taasisi ya E3 empower Afrika amesema maonesho hayo yamelenga kutoa elimu ya sayansi na kuwahamasisha wanafunzi kuweza kupenda masomo hayo,ili kuwajenga vijana kifikra kwani mwamko katika masomo ya sayansi ni mdogo kuanzisha shileni hadi vyuoni.
"Tikianza kuwaonyesha mambo muhimu ya sayansi wanaweza kushawishika na wakaws mabalozi wa wenzao katika kuwapa mwamko wa masomo ya sayansi kwa nchi yetu."Alisema Mwezeshaji huyo
Pamoja na hayo amesema E3 empower Afrika ni Taasisi inayojitegemea na kujishughulisha na utoaji wa elimu ya masuala ya Teknolojia kwa vijana ndani ya jamii ambapo tayari taasisi hiyo imewafikia vijana wengi hususani wanafunzi kuanzia shule za msingi,sekondari,vyuo na wale ambao hawakupata nafasi ya kupata elimu rasmi.
"Teknolojia tunazowapa ni teknolojia ambazo kwenye masomo yanayofudisha shuleni huwa wahapati,maana sisi tunafundisha masomo ya sayansi,teknolojia ,uhandisi na mahesabu ambayo kwa ujumla wake tunakuwa na kozi ambazo zipo kwenye masuala ya teknolojia,uhandisi na kwenye masuala ya mahesabu."alisema George
Vilevile amesema wanawafundisha vijana namna ambavyo dunia inaweza kuona nguvu kazi za watu zimechukuliwa nafasi na mashine bila kuendeshwa na nguvu za binadamu,pia wanawafundisha wanafunzi jinsi ya kutengeneza alamu ya kuashiria hatari za moto,namna ya kutengeneza application za simu na web site.
Ameongeza kuwa ufundishaji wa masomo ya sayansi mashuleni kwa nadharia kunawafanya wanafunzi kutokuwa na uelewa wa wapi watayatumia maarifa hayo hivyo ufundisha wa vitendo katika masomo hayo kutawajengea msingi wa fikra.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya E3 empower Afrika,Ji-Young Yoon Rhee amesema lengo lao ni kutoa elimu kwa watoto wa kitanzania kuanzia ngazi ya msingi,sekondari hadi vyuo ili kukuza teknolojia ya sayansi kwa wanafunzi wa kike ambapo program hiyo imeanza kwa kutoa elkmu katika shule ya Sekondari ya Arusha Girls.
Ameongeza kuwa program hiyo ambayo niya miaka 3 hadi mwaka 2023 chini ya Ufadhili wa KOICA imelenga kufikia shule zote za serikali za wasichana Mkoani Arusha ambapo tayari wanafunzi wa kike wapatao 100 wasio katika mfumo wa elimu rasmi wamepatiwa elimu hiyo .
0 Comments