Header Ads Widget

KIJANA AFARIKI DUNIA KWA KUJITOSA BAHARINI

 


NA HADIJA OMARY MATUKIO DAIMA APP ,LINDI

KIJANA Moja Hassan Mbuyu Mkazi wa mtaa wa sabasaba Manispaa ya Lindi,  Hassan Mbuyu mwenye umri wa miaka 27  amefariki dunia baadada ya kujitosa baharini katika fukwe za bahari ya hindi

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa oilisi mkoa wa lindi Mtatiro Kitinkwi alisema kuwa tukio hilo lilitokea hapo jana April 4 majira ya saa12:30 jioni  eneo la sea viw hotel iliyopo Manispaa ya Lindi

Alisema uamuzi wa kijana huyo kujitosa baharini ni katika harakati za kukimbia mkono wa Sheria baada ya Mpenzi wake Sharifa Zakaria kwenda nae kituoni kuitikia wito baada ya kumripoti kuwa amempiga na kumtishia Maisha


Kitinkwi alisema baada ya Wawili hao kufika kituoni wakati kijana huyo akihojiwa na asikari wa zamu alikimbia kutoka kituoni kwa kuhofia kuwa atawekwa ndani  na kukimbia baharini na kujitosa majini.

Hata hivyo kitinkwi alisema kuwa juhudi za uokoaji zilifanyika kupitia kikosi cha uokoaji na zima moto ambapo leo April 5, 2022 majira ya kikosi hiko kilifanikiwa kuupata mwili wa kijana huyo  katika eneo ambalo alijitosa akiwa akiwa tayari amefariki dunia

Kwa upande wake Daktari wa zamu  hospitali ya Rufaa Sokoine Daud Craver amethibitisha kupokea mwili wa marehemu huyo ambapo amesema kuwa uchunguzi unaonyesha sababu ya kifo chake kugongwa na kitu chichwani kulikopelekea majelaa katika eneo la kichwa , shingo na kwenye taya

“ tulipokea mwili wa marehemu majira ya saa tatu asubuhi baada ya uchunguzi tuligundua marehemu huyo alikuwa anatokwa na damu puani na mdomoni ambayo ilikuwa imechanganika na mapovu lakini pia shingo yake ilikuwa inaonekana imelegea kwa hivyo inaonyesha kwamba aliumia aidha alivunja shingo lakini pia kutokwa hizo damu inawezekana chini ya fuvu la kichwa”

“Hata hivyo kulingana na uchunguzi wa ndani tulioufanya kwa marehemu huyu , tumeangalia tumboni na kwenye mapafu yake lakini hatukumkuta na maji  wala kitu chochote ambacho kinaashiria kuwa marehemu hiyo alikufa ndani ya maji”


Akizungumzia tukio hilo Sharifa Zakalia ambae pia ni Mpenzi wa Marehemu huyo alidai kuwa wawili hao walikuwa na ugomvi ambao ulisababisha shalifa kutaka kuachana na mpenzi wake huyo ambapo siku chache baadae Hassan ambae ni Marehemu aliamua kupinga uamuzi wa mpenzi wake kutaka waachane

 

Sharifa alisema baada ya maamuzi yake ya kutaka kumuacha mpenzi wake huyo ndipo Hasani alianza kumsaka kwa baadhi ya watu wa karibu wa sharifa ndipo usiku wa tarehe tatu akamchukuwa binti huyo kumpeleka moja kwa moja nyumbani kwake kuanza kumvua nguo na kumpiga

“kwa kuwa alisha anza kunitishia Maisha niliona bora niondoke nyumbani niende kuishi kwa Rafiki yangu mtaa wa mikumbi ambako baada ya kugundua kama nipo kule usiku wa kuamkia juzi alinifuata na kuniamuru nipande kwenye boda boda yake tuende nyumbani kwake tukayazungumze, kwa kuondoa fujo kwenye majumba ya watu nikaona nimkubalie kuondoka nae”


“hata hivyo baada ya kwenda kwake alinivua nguo zote na kunipiga kisha kunitishia kuniua, baada ya tukio line usingizi ukampitia baadae nikaamua mkutoroka kwenda nyumba ya jirani na palivyokucha  nikaenda kituo cha polisi kushitaki kisha kupewa barua ya Wito ili afike kituoni”

 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI