Na Fatma Ally Matukio Daima APP, Dar es Salaam
Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia leo imegawa kompyuta, 3,354 kwa ajili ya wadhibiti ubora wa shule, maafisa elimu Kata ,shule za Sekondari pamoja vyuo vya ualimu.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa vifaa hivyo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa, komputa hizo zitagawiwa kwa maafisa Uthibiti ubora na Maafisa Elimu Kata ili kuboresha utendaji kazi wao ambapo vifaa hivyo vimenunuliwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa elimu.
Aidha, amesema kuwa vifaa vilivyo zinduliwa ni pamoja na kompyuta 3,354 ambapo kati ya hizo Laptop ni 1637 na Deskotop kompyuta ni 1717, printer 12, projector 12 na internet switches 12, Desktop kompyuta 1717, Laptop 300, ambapo Vifaa hivyo vimetolewa na Shirika la “Digital Pipeline” la nchini Uingereza na vitasambazwa katika shule za Msingi, Sekondari na vyuo vya ualimu.
Sambamba na hayo pia wamenunua vifaa vya kisasa vya studio kwa ajili ya kufanya recording ya vipindi kwa njia ya radio, TV ili kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji wakati wa majanga, kuchapa vitabu vya maandishi yaliyokuzwa na Braille kwaajili ya wanafunzi wasioona na wenye uoni hafifu ili kuboresha ufundishaji na usomaji wa wanafunzi hao.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Gerald Mweli amesema wanafahamu mtaala wa elimu ya TEHAMA ulianzishwa zamani na unatekelezwa lakini hawakuwahi kuwa na vifaa vingi kama ambavyo vimetolewa leo, kwa maana hiyo vifaa hivyo vitasaidia sana katika Utoaji wa Elimu bora zaidi.
Mmoja wa wanufaika wa mradi wa kuboresha mazingira, Michael Cheyo kutoka Kanda ya Kusini amesema kupewa kompyuta mpakato ni fursa nzuri kwasababu sehemu kubwa ya utendaji kazi wao ni vifaa hivyo hivyo wanaahidi kufanya kazi Kwa wakati bidii kwa kuboresha kazi kufikia malengo.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake mwanafunzi aliyeshiriki katika ugawaji wa vifaa hivyo, ameishukuru Wizara kwa kuwapa vifaa hivyo ambavyo ni kompyuta mpakato kwa ajili ya Udhibiti ubora wa shule ya Sekondari zitawasaidia katika kurahisisha kazi na kusaidia kuwa mzalendo wa nchi, kuendeleza ujuzi na kufikia malengo.
Aidha, ameahidi watavitumia vifaa hivyo kwa ufasaha ili watakapomaliza masomo wanafunzi watakaokuja kuendelea waweze kuzikuta na wao wazitumie kwa kuongeza ujuzi zaidi.
0 Comments