Header Ads Widget

MRADI WA KITUO CHA AFYA BARIKIWA KUNUFAISHA WAKAZI 8,158

 


NA HADIJA OMARY _LINDI


JUMLA ya wakazi 8,158 kutoka kutoka katika kata mbili za Barikiwa na Mkutano Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi wamepata tumaini jipya la upatikanaji wa huduma za afya jirani na maeneo yao  baada ya mwenge wa Uhuru 2022  kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Kituo cha Afya Barikiwa.



Wakizungumza na Matukio Daima mara baada ya kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kuweka jiwe la Msingi katika ujenzi huo  baadhi ya akina mama akiwemo Mwanahawa  Ngojwike alimshukuru  Rais Samia kwa uwamuzi wake wa kutenga fedha kwa ajili ya kituo hiko cha afya ambacho kilikuwa kilio chao cha muda mrefu



Alisema changamoto wanayokabiliana nayo kwa sasa kwa kutokuwa na huduma za afya jirani na maeneo yao hasa ni kwa akina mama wajawazito kujifungulia njiani wakati wakielekea kupata huduma za Afya nje ya maeneo yao ama kujifungulia kwa mkunga wa jadi ili kukwepa gharama za usafiri na kuishi mbali na maeneo yao jambo ambalo ni hatari kwa mtoto na mama kwa ujumla



Nae Mwanaesha kumchenyenda aliiomba Serikali baada ya ujenzi huo wa awamu ya kwanza kukamilika kuharakisha umaliziaji wa majengo ya akina mama kujifungulia kwa kuwa wao ndio wahanga wakubwa katika changamoto hiyo.



" wakati mwingine tunashindwa kwenda kwenye hospital ya Wilaya kuogopa gharama, wakati mwingine uchungu unakuanzia usiku na hakuna gari muda huo, kutoka hapa mpaka liwale mjini nauli kwa boda boda sio chini ya shilingi Elfu 5000 kwenda tuu na hiyo ni nauli ya mchana sikuambii usiku kwa misha ya sasa kweli tutaweza?"  Alihoji kumchenyenda




Akizungumza na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika kituo hiko Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa   mwaka 2022 Sahili Geraruma   alimtaka msimamizi wa ujenzi  wa kituo hiko kukamilisha ujenzi huo kwa wakati uliopangwa  na kwa viwango vinavyotakiwa ili uanze kutumika na wananchi hao.



Alisema Ili fedha ya Serikali iliyotolewa kwa ajili ya ujenzi wa kituo hiko cha afya ni wananchi kupata huduma zinazostahiki kwa wakati uliopangwa



Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa kituo hiko mtendaji wa kata ya Barikiwa kelvin Msuha alisema ujenzi huo mpana kukamilika kwake unatarajia kughalimu kiasi cha shilingi 250,000,000. Ulianza utekelezwaji wake terehe 10 january mwaka huu ukihusisha jengo la Wagonjwa wa nje, (OPD) Maabara, pamoja na kichomea taka ambao unatarajia kukamilika mwezi juni 2022



Msuha alieleza kuwa uwepo wa kituo hiko kitawafanya Wananchi wa maeneo hayo kupata huduma kwa wakati ukilinganisha na sasa ambapo wananchi hao ulazimika kutembea umbali wa kilometa 40 hali inayopelekea kuhatarisha maisha ya wagonjwa pia kumuongezea gharama za kuishi anapokuwa mbali na makazi yao.



"Kwa sasa  Usafiri ikitokea  mama mjamzito akapata  changamoto  tunaomba Gari ya ambulance kutoka hospital ya wilaya ambayo nayo kwa sasa  ipo moja tu kwa kata 16 zilizopo kwenye halimashauri hii" alifafanua Msuha.



Post a Comment

1 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS