Header Ads Widget

MFANYAKAZI WA KULISHA NG'OMBE ATUHUMIWA KUUA MFANYAKAZI WA NDANI

 


MFANYAKAZI wa kazi za kulisha ngombe (27) ambaye jina lake limehifadhiwa anashikiiwa kwa tuhuma za kumuua msichana wa kazi za ndani kwenye nyumba walikokuwa wakifanya kazi.


Kamanda wa Polisi mkoani Pwani ACP Pius Lutumo amesema kuwa mtuhumiwa na marehemu walikuwa wakifanya kazi kwa mtu aliyefahamika kwa jina moja la Samwel.


Lutumo amesema kuwa mtuhumiwa ambaye jina limehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi (27) alimuua Dawiya Mshihiri (30) kwa kumshambulia na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili.


Amesema kuwa mtuhumiwa baada ya tukio hilo alijaribu kujiua kwa kunywa sumu lakini hakufanikiwa na kukamatwa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi kwa matibabu akiwa chini ya ulinzi wa Polisi.


Aidha amesema kuwa mtuhumiwa na marehemu walikuwa wakifanya kazi kwenye nyumba moja na Polisi wanaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.


Kamanda Lutumo amesema kuwa mara upelelezi utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria na nawasihi wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI